Tuesday, 18 February 2020

RIPOTI YA FEDHA YASOMWA BUNGENI EALA LEO

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Bunge la Afrika mashariki EALA limeanza kikao chake leo leo kwa kusomwa  ripoti ya Fedha ya mwaka 2017/18 ambayo iliwasilishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Fedha na Mipango ya bunge.

Akiwasikilisha bungeni humo mapema mchana wa leo kwenye  kikao cha tatu cha bunge la nne Dkt.Ng'waru Maghembe alisema kuwa jumuiya hiyo kwa mwaka huu imepata hati safi baada ya mwaka uliopita kupata hati chafu kutokana na makosa ya kifedha.

Alieleza kuwa kumukuwa na changamoto kadhaa za ajira za muda ambazo zinahitajika kuangaliwa ili kuendana na mikataba ya ajira za watumishi ambazo zitaongeza ufanisi kwenye utendaji 

Akataja sababu zilizopelekea jumuiya hiyo kupata hati safi ikiwa ni pamoja na kulifanyiakazi suala zima la kuweka ripoti za kifedha  pamoja kuonyesha matumizi japo bado kuna changamoto kidogo ambazo zikishughulikiwa zitaleta manufaa zaidi.

Alisema kuwa japo michango ya nchi wanachama haijakidhi bajeti bado sio muda muafaka wa kuangalia hilo tuangalie Sana kwenye mtangamano na Faida zake kwa nchi zetu.

No comments:

Post a comment