Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

 NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Gerald Mweli amewapongeza walimu wa shule ya Sekondari ya Dodoma kwa kupandisha ufaulu na kuwataka kufuta zero na daraja la nne katika mtihani wa mwaka huu wa kidato cha nne.

 Aidha, Mkuu wa shule hiyo, Amani Mfaume amemuahidi Naibu katibu Mkuu kama hatafuta ziro kwenye mtihani ujao basi atajiuzulu wadhifa huo.

 Akizungumza mara baada ya kuzungumza na walimu wa shule hiyo, Mweli alisema uongozi wa shule hiyo umefanya mabadiliko makubwa kwa kuongeza ufauli na kutolea mfano kuwa kwa matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa mwaka huu, ziro zimepungua hadi kufika 19 kutoka 67 zilizokuwapo katika wanafunzi waliomaliza mwaka 2018.

 Alisema pia wanafunzi waliopata Daraja la I katika matokeo ya mtihani wa mwaka 2019 zimefikia 13 kutoka 5 za mtihani wa mwaka 2018 huku wasichana wakiwa 6 na wavulana 7.

 Mweli alisema wanafunzi 32 waliopata Daraja la Pili ikilinganishwa na wanafunzi 20 kwa mwaka 2018 huku wanafunzi wa kike wakiwa saba na wavulana 25 wakati wanafunzi 49 wamepata Daraja la Tatu kutoka wanafunzi 36  wa mwaka 2018.

“ Nimekuja kuzungumza na walimu wangu, hwana ndio majembe yangu, nimekuja kwanza kutambua kazi nzuri waliyoifanya ya kuongeza ufaulu pamoja na kuwa na changamoto.

“Kwa kuongeza wanafunzi waliofanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza inamaana wameongeza, wahandisi, au fani zingine, hivyo nikaona nije kuwapongeza lakini kubwa tumekubaliana na kuwekana na mkataba wa kufuta ziro na division four.

 Aidha, Mkuu wa shule hiyo, Mfaume alimuahidi naibu katibu mkuu kuwa endapo hatazifuta ziro katika mitihani wa kidato cha nne unaokuja basi atajiuzul wadhifa wake huo.
Haya hivyo walimu wa shule hiyo pamoja na kubainisha changamoto kadhaa ikiwamo ya tabia ya wanafunzi kudharau baadhi ya masomo, waliishukuru Serikali kwa maboresho yaliyofanyika na kuiomba kusaidia kuboresha makataba ya sasa ili kuwa na makataba mtandao ambayo itawawezesha wanafunzi kupata na kusoma vitabu vingi kupitia tekinolojia hiyo.

 Aidha, Mweli ambaye alikubali kuwa mlezi wa shule aliahidi kuzitatua baadhi ya changamoto na zingine kuziwekea mikakati ya pamoja katika kuzitatua.
Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: