Friday, 21 February 2020

MDAU WA WATU WENYE UALBINO JOSEPH GORYO ATOA MISAADA SHULE YA MITINDO, MWANZA

Mdau wa maendeleo Mwanza Joseph Goryo akiwa na watoto wenye albino baada ya kuwapatia msaada 

MDAU mkubwa wa mambo ya jamii ikiwemo elimu kwa wanawake, Watoto  na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) Joseph Goryo ametoa misaada mbalimbali shule ya msingi Mitindo iliyoko Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Misaada hiyo ni pamoja na  kandambili PC 100, mashuka 104, masweta ya shule 25, Sketi 10 na miwani kwa watoto wenye ualbino wanaolelewa na kusomea shule hiyo.

Akikabidhi misaada hiyo, Goryo amewaomba wadau mbalimbali kuitembelea shule ya msingi Mitindo na kuwasaidia watoto hao ambao kwasasa wanamahitaji mengi.

"Tupatapo kikubwa ama kidogo tuje kwa wingi kuwasaidia watoto wetu

Hitaji lao kubwa ni dawa ya meno, miswaki,madaftali, kalamu pamoja na kofia za kujikinga na jua na vingine  maalum ikiwemo t-shit." Alisema Goryo.

Goryo aliongeza kuwa watu wenye misaada wanaweza kufika shuleni hapo na kuonana na uongozi wa shule na itapokelewa kwa moyo mmoja hata kama ni kidogo.

Shule hiyo ya mitindo ina Watoto wenye ualbino 113 ambapo Wavulana 54 na Wasicnana 58.

Wengine ni watoto wenye tatizo la Ukiziwi (Viziwi) ambao wapo 110. Kwa maana Wavulana 55  na wasichana 55.

Kwa upande wa watoto Wasiona Wavulana 23 na Wasichana 26 na kufanya idadi yao kuwa, 49.

Mbali na hao pia shule hiyo ina watoto wanaotoka Mazingira magumu Wanne huku wa kiume akiwa mmoja na wa kike wakiwa watatu.

Jumla kuu ya watoto hao ni wavulana 133 na wasichana  142 na kufanya jmla ya  watoto wote kuwa 275.

Mwisho

No comments:

Post a comment