Huu ni muonekano wa  Stendi kuu mkoa wa Arusha. Picha na Vero Ignatus)

Na.Vero Ignatus,Arusha

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini mkoa wa Arusha (LATRA)inaenaendelea na ukaguzi maalum wa magari ya abiria na malori ya kusafirsha mizigo ambayo hayana leseni na kuyachukula hatua za kisheria.

Akizungumza kuhusiana na zoezi hilo Afisa Mfawidhi wa mkoa wa Arusha Leyla Daffa amesema kuwa Zoezi hilo lililoanza jumanne ya wiki iliyopita katika maene tofautitofauti ya Jiji la Arusha pamoja na wilaya zake ambapo wameweza kukamata magari yenye makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya kutokuwa na leseni.

LATRA ilifanya ukaguzi katika wilaya ya Longido na Arusha mjini katika stendi kuu ya mabasi,Stendi ya Kilombero,Samunge na stendi ndogo  daladala ambapo kwa(W) Arusha mjini wamekamata daladala 10 (W)Longido malori 7 na mabasi 3 ambapo wamewachukulia hatua za kisheria ikiwemo kulipishwa faini

Daffa alisema magari mengi yaliyokamatwa yameadhibiwa kwa kulipa kiasi cha shilingi laki mbili na nusu kwa kila ambaye alikamatwa kwa kutokuwa na leseni ya LATRA kama sheria inavyoelekeza

Aidha zoezi hilo ni endelevu kwa maeneo mengineyo haswa katika wilaya za pembezoni katika mkoa wa Arusha zilizobakia ambazo ni Monduli,Karatu,Arumeru

Ametoa wito kwa wasafirishaji wote kuhakikisha kuwa wanaenda kufanya maombi ya leseni mapema iwezekanavyo punde tu wanapobaini leseni zao zinakaribia kwisha kwani wasipofanya hivyo Mamlaka hiyo itakamata magari hayo na hatua nyingine za kisheria zitafuata ikiwemo kulipa faini ama kupelekwa Mahakamani

Madereva  wanaotumia barabara ambazo zipo katikati ya makazi ya watu LATRA imewataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani atakaye kamatwa akifanya vitendo hivyo vya kukaidi na uvunjifu wa sheria  hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake

Aidha Mamlaka ya Udhibiti Ardhini LATRA kwa mujibu wa kifungu cha 5(1)(b)cha sheria ya LATRA namba 3 ya mwaka 2019 kutoa na kusimamia leseni za usafirishajibabiria na mizigo ardhini ni jukumu la LATRA

Hivyo Mamlaka hiyo imeweka utaratibu wa kutoa leseni katika ofisi za Mikoa yote Tanzania bara hivyo mtu yeyote atakayesafirisha abiria bila leseni ya Mamlaka husika atakuwa amevunja sheria ya LATRA kifungu cha 5 (1)(b) na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake


Mwisho
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: