Kamati ya Siasa Wilaya ya kichama ya Meru, Arumeru  imeridhiahwa na mradi wa ujenzi ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Elikirimuni Kata ya Ngarenanyuki Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kueleza kuwa Serikali kupitia Arusha National Park (ANAPA) imetekeleza vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM ibara ya 50 inayoielekeza Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi wake katika umbali mdogo. 


Haya yamejiri Siku ya Kwanza ya ziara ya kamati hiyo kwenye Halmashauri ya Meru ambapo Katibu  wa CCM Wilaya ya Arumeru Ndg. Gurisha Mfanga  amepongeza hatua za ujenzi wa zahanati hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni 125,285,805 ikiwa kiasi cha Milioni 87,700,063.50 ni fedha kutoka ANAPA na Shilingi Milioni 37,585,741.50 ni michango ya Wananchi. Pia ameielekeza Halmashauri kupeleka huduma  ambazo zinaweza kutolewa wakati ukamilishaji unaendelea  na kuhoji  mchango wa Halmashauri kwenye ujenzi huo ikizingatiwa ni Kata ya pembezoni. 



Akitoa ufafanuzi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg. Emmanuel J Mkongo  ameahidi kufanyia kazi maelekezo ya Chama na kueleza kuwa kwa mwaka wa fedha uliopita  2018/2019 kila Kata ilipewa Shilingi Milioni kumi kwaajili ya miradi ya Maendeleo ikiwepo Kata ya Ngarenanyuki pia Halmashauri imehakikisha Mradi huo unajengwa kwa viwango kupitia Mhandisi wa ujenzi . 



Naye Mheshimiwa diwani wa Kata ya Ngarenanyuki Zacharia Nnko kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki hususani Kijiji cha Elikirimuni ameishukuru Halmashauri kwa ufunguzi wa barabara kuelekea kituoni hapo "ufunguzi wa barabara hii ni mwangaza kwa zahanati hii kwani bila Halmashauri kuleta mtambo (na kufungua barabara hii tusingeweza kufika hapa leo hii"Amefafanua Mhe.Zakaria 



Katibu tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Nchembe ametoa wito kwa Viongozi wa Kata na Vijiji  kuwajengea uelewa wananchi ili waweze kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo "sisi sote ni watanzania hatuna budi kujiletea maendeleo kwa kuchangia ujenzi wa  mradi huu wa afya maendeleo hayana mipaka " amesisitiza Mwl. James 



Aidha ziara hiyo imekamilika kwa Siku ya kwanza kwa Kukagua Mradi wa ujenzi wa Kijiji cha Elikirimuni na Jengo la  Wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya kijiji cha kwa ugoro ambapo Chama  kimeielekeza Halmashauri kuongeza idadi ya Watumishi katika zahanati ya Kwaugoro sambamba na Watumishi wa zahanati hiyo kuhakikisha kunakwepo na usafi wa kuridhisha .

Jengo la Zahanati ya Ilikirumuni.
Mtendaji wa Kijiji cha Ilikirumuni akitoa ufafanuzi wakati wa ukaguzi.
ukaguzi jengo la zahanati Ilikirumuni.
Katibu wa CCM akitoa maelekesho  ya kutoa huduma za afya katika Jengo la Zahanati ya Elikitumuni.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashairi ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa ukaguzi wa Jengo la Zahanati ya Elikirumuni.
Katibu tawala Wilata ya Arumeru akizungumza wakati wa ukaguzi wa Jengo la Zahanati ya Elikirumuni.

Kamati ya siasa ikiwa katika Zahanati ya Kijiji cha kwaugoro.
Jengo la mama na mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha Elikirumuni.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kichama Meru ,Ndg.Gurisha Mfanga.


KATIBU tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.JamesNchembe akisisitiza uzalendo kwa Watumishi wa Zahanati ya Kwaugoro.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: