Tuesday, 28 January 2020

WAKULIMA SONGEA WALIA NA UHABA WA MBOLEA YA UREA KUKOSEKANA

 Baadhi ya Wakulima wakiiomba kuangalia namna ya upatikanaji wa mbolea aina ya Urea .

Hali ya mazao ilivyo shambani 

 BAADHI ya Wakulima wa Songea mkoani Ruvuma wameiomba Serikali ya Wilaya na Mkoa  kukaa meza moja ya mazungumzo na mawakala wa usambazaji wa pembejeo kwa wakulima ili kuzuia adhari isijitokeze kwa wakulima.mwandishi Amon Mtega anaripoti kutoka Ruvuma

  Ombi hilo wamelitoa juzi wakati wakizungumza na Msumbanews kuhusiana na  changamoto ya upungufu wa mbolea aina ya Urea ambayo inadaiwa kuadimika kwenye mkoa huo na kuwafanya wakulima hao kuhangaika namna ya kuipata.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja wa wakulima Firbet Komba ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mbingamharule  Wilaya ya Songea amesema kuwa kunakila sababu ya Serikali ya Wilaya na mkoa kukaa meza moja na mawakala hao ili kutatua changamoto zilizopo hasa za uadimikaji wa mbolea ya Urea ambayo inaongoza kutumiwa na wakuliama wengi mkoani humo .

  Amesema kuwa hadi sasa mbolea hiyo imekuwa ikipatikana kwa shida na kama ikipatikana imekuwa haiwatoshelezi wakulima jambo ambalo alidai kuwa limekuwa linawapa hofu wakulima hao kuharibika mazao yao (Mahindi) kwa kukosa mbolea hiyo.

 Kwa upande wake mmoja wa mawakala wa usambazaji wa pembejeo hizo Wilayani humo Tito Mbilinyi(Mwilamba)amesema kuwa tatizo la upatikanaji wa mbolea aina ya Urea ni kubwa hivyo mawakala wamekuwa wakihangaika namna ya kufanikisha kuzipata ili kuokoa mazao ya wakulima.

 Mbilinyi amesema kuwa inafikia wakati baadhi ya wahitaji wamekuwa wakiwalalamikia wasambazaji wakidhani kuwa labda mbolea hiyo imefichwa kwa kutaka kuiuza bei ya juu tofauti na maelekezo ya Serikali ,kumbe sivyo.

  Amesema kuwa kufuatia changamoto hiyo ya ukosefu wa mbolea ya Urea ,mawakala wapo tayari kukaa meza moja na uongozi wa Serikali na Wilaya ili kulitatua tatizo hilo na kuwafanya wakulima waweze kupata huduma ya pembejeo.

Ameeleza  kuwa yeye anasambaza pembejeo katika Vijiji zaidi ya kumi vilivyopo Wilaya ya Songea na vya Wilaya ya Namtumbo kwa kuwapelekea kwenye maeneo yao ili kuwapunguzia adha wakulima hasa wenye mitaji midogo.

               

No comments:

Post a comment