Mhandisi wa wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kadaya Baluhye akizungumza na Mafundi wa simu kutoka mkoa wa Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo aliwataka kuunda umoja wa kikanda leo tarehe 28/1/2020
Maguwa Manyanda Mwenyekiti umoja wa Mafundi simu Kanda ya ziwa akizungumza katika kikao cha Mafundi simu kulichoandaliwa na Mamlaka ya mawasiliano TCRA
Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Kant Mosha akizungumza na Mafundi wa simu kutoka mkoa wa Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo aliwataka kuunda umoja wa kikanda
Mmmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia mada katika mkutano huo wa mafundi simu uluioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano 
 Mhandisi Jan Kaaya TCRA Kanda ya kaskazini ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Imelda Salum,akizungumza na Mafundi simu waliohudhuria kuikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa leo.
Jemsi Moshi mmoja wa Fundi simu mkoa wa Arusha ambae pia yupo kwenye kamati ya uongozi wa katika kikao cha mafundi simu kilichoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA.
Joyce Mmari fundi (simu)na Inyasi Mpaki ambae ni mwenyekiti wa mafundi simu Manyara ambao pia ni washiriki  wa mkutano  ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kanda ya Kaskazini lna kufanyika leo katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Jijini Arusha

Mhandisi Jan Kaaya TCRA Kanda ya kaskazini akiwa ameshika jarida ambalo amewataka  Mafundi simu waliohudhuria kukao hicho kulipitia na kuona kanuni na taratibu pamoja na Maelezo ya kina kuhusiana na TCRA katika mkutano kil
uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa leo.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mafundi simu ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini uliofanyika leo Jijini Arusha katika ukumbi nwa mkuu wa mkoa.
 Nasri Ramadhani Mshana mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi wa Simu Kanda ya Kaskazini akizungumza na na Mafundi simu katika mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA
 Mhandisi wa wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kadaya Baluhye akizungumza na Mafundi wa simu kutoka mkoa wa Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo aliwataka kuunda umoja wa kikanda
 Mhandisi wa wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kadaya Baluhye akizungumza na Mafundi wa simu kutoka mkoa wa Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo aliwataka kuunda umoja wa kikanda
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mafundi simu ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Kaskazini uliofanyika leo Jijini Arusha katika ukumbi nwa mkuu wa mkoa leo tarehe 28/1/2020


 Na, Vero Ignatus Arusha

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kanda ya kaskazini imewataka mafundi wa vifaa vya kieletroniki ikiwemo simu za mikononi kuwa kwenye mfumo wa umoja kwa kuanzisha vikundi vyao kwa kanda hiyo au kwa mikoa yao.

Kwa muktadha huo kuanzia mwezi julai mwaka huu hakuna fundi ambaye atafanyakazi kama hajasoma hivyo ni muhimu kwenu kujiunga ili muweze kupatiwa elimu ya ufundi tena bure.

Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria wa mamlaka hiyo Kant Mosha wakati wa mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo aliwataka kuacha kutokuwa na usajili wa kikundi kwa kuwa kikundi ndio suluhisho.

Alisema kuwa umoja ndio nguzo muhimu kwao ambapo itawasaidia kuepusha kuonewa na wateja wao,kuwa na maelngo ya pamoja kusaidiana kwenye changamoto zao mbali mbali badala kuwa mtu mmoja kwa kuwa sisi ni thamani.

Alisema kuwa mafundi simu ni kada ambayo ilikuwa imesahaulika hapo awali lakini serikali ya awamu tano imeamua kuwatambua hivyo kuungana ni sehemu ya kufanikiwa kwenye malengo yenu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mafundi simu Kanda ya ziwa Maguwa Manyanda amewataka kutambua kwamba mafundi simu ni wa thamani kwani jamii inawategemea na wanachangia pato la taifa hivyo busara ni kuona umoja ndio suluhisho la changamoto za mafundi simu.

Alisema kuwa Mafunzo hayo yataondoa changamoto zao na kuwafanya kuwa huru katika shughuli zao za kila siku,hivyo umoja ni nguzo ya kuwafikisha kuweza kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ikiwemo vymbo vya dola.

Alisema kuwa kufanikiwa kwao lazima kuungana na kuwa kitu kimoja kwa kutambulika na mamlaka ya mawasiliano kwa lengo la kuweza kupata mafunzo mbali mbali yatakayotolewa na kada mbalimbali.

Nae Mhandisi wa TRCA Kadaya Baluhye alisema kuwa ni vyema mafundi wa simu wakawa na elimu ya kile wanachokifanya ili mamlaka ikitoa vyeti itoe kwa mtu aliepata ujuzi.

Alisema kuwa umuhimu wa umoja wao utasaidia kuondoa kadhia mbali mbali ambazo zingeweza kuwakumba kwa kuwa tutawafahamu mafundi wote na kuweza kuwapa elimu ambayo ni bure kwa mafundi hao.

Nao baadhi ya washiriki kwa (umoja wao)katika mkutano huo wameiomba Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la kuwapa ushirikiano kwani baadhi ya mafundi wa simu wanawafahamu baadhi ya watu ambao siyo waaminifu katikati ya jamii ambao wanapora simu na kwenda kuwauzia hivyo watakapowapa ushirikiano ni rahisi kutokomeza tatizo hilo katika jamii.

Pia wameliomba Jeshi la Polisi Kanda ya Kaskazini kuhudhuria katika vikao vyao ili waweze kuwasikiliza pale wanapotoa malalamiko yao pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kiufundi kwa wateja wao kila wakati.

Mwisho.

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: