Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma kutoka Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani ( RSA) Ally Nurdin  

Na.Vero Ignatus,Pwani.
Taasisi ya Mabalozi wa usalama barabarani (RSA)kwa kushirikiana  na wadau wengine wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya usalama barabarani nchini Tanzania iliyotungwa mwaka 1973 ambapo sheria hiyo imerithi kanuni mbalimbali zilizotungwa tangia mwaka 1933 ambapo zimeendelea kuboreswa kipindi hadi kipindi.
Akizungumza Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma( RSA) Ally Nurdin  amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2018 marekebisho makubwa ya sheria hiyo ya usalama barabarani sura ya 168 ni yale ambayo yalifanyika mwaka 1996.
''Marekebisho hayo yalifuata baada ya hapo yalihusu ongezeko la faini tu bila kugusa vipengele vya msingi vya sheria yenyewe kwasababu tangu wakati huo hadi sasa idadi ya magari inaongezeka barabarani idadi ya watumiaji wa vyombo vya moto inaongezeka pamoja na vyombo tofautitofauti ambavyo havikuwepo wakati huo pia vinatumika barabarani na tabia za watumiaji wa vyombo hivyo zinabadilika kwa kuongezeka tabia nyingi mpya ambazo hazikuwepo''Alisema
Nurdin alimesema kuwa vipengele vinavyotakiwa kufanyiwa marekebisho ni pamoja na kifungu cha 5 kuhusu usajili wa magari lakini hakiweki wazi iwapo usajili huo ni ule wa kieletroniki ili mmiliki wa gari asilazimike kutembea na gari muda wote,kwasababu kadi inaweza kuwepo mkwenye simu au kwenye App fulani,ambapo sheria ni wakati wake kutambua jambo hilo.
Amesema kuhusu umri wa kumiliki gari kifungu cha 10(20)sheria ilivyo sasa inamapungufu inampiga marufuku mtu aliye chini ya miaka 18 kumiliki gari hata hivyo aliye na miaka 14 anaruhusiwa kumiliki pikipiki,amesema yapo maoni kwamba sheria hiyo isiruhusu kabisa aliye chini ya miaka 18 asimiliki pikipiki wala gari japo kuwa maoni mengine yanakinzana na kusema aruhusiwe.
''Swali linakuja je mmiliki akitaka kuuza atauzaje wakati kuna mikataba inayosema kuwa aliyechini ya miaka 18 haruhusiwi kui ngia katika mkataba,wakati huo huo ikitokea kwamba kuna makosa yanamhusu mmiliki wa gari kushtakiwa au kufungwa au kulipa faini je atalipaje kwa mmiliki wa umri wa chini ya miaka 18?'' Aliuliza 
Aidha amesema kuwa katika faini kutumia gari bila kusajili sheria hiyo katika kifungu cha 8(2) ambapo faini yake ni shilingi elfu hamsini tu au kifungo kisichopungua miaka mitano,amesema faini hiyo italipwa mahakamani iwapo mtuhumiwa atakutwa na hatia,jambo ambalo barabrani faini yake ni shilingi elfu thelathini.
Amesema kuwa kifungu cha 11(4)kuharibu au kubadili alama za utambulisho wa gari inamtaka alipe faini ya shilingi elfu kumi ambapo adhabu hiyo ni ndogo kwa wanaofanya makusudi ili wasitambulike wanapofanya makosa,amesema kifungu cha 14(5) kosa la kutoweka au kuficha alama ama kuongeza alama za utambulisho wa gari adhabu yake ni shilingi elfu tano ambapo haimfanyi mhusika kuijutia kosa.
Aidha Amesema kifungu cha 18 kinahusu kosa la kutumia gari bila alama za utambulisho au kutumia alama za utambulisho wa gari lingine au kutoa taarifa za uongo kuhusu usajili wa gari ambapo kosa hilo kwa sasa adhabu yake shilingi 10,000 Kwani makosa ya makusudi kama haya adhabu yake ni ndogo,kifungu cha 19 kosa la kuendesha gari pasipokuwa na leseni halali au kumruhusu asiye na leseni adhabu ya kosa hilo nayo ni shilingi 10,000
Ameainisha kuwa kifungu cha 21(1) leseni ya lena kwa dereva mwanafunzi wa udereva wa pikipiki amesema sheria iliyop[o sasa haimlazimishi anayejifunza kukata leseni ya lena kabla ya kuanza kujifunza kuendesha hivyo ni vyema seria ikaweka hitaji hilo kwa madereva wa pikipiki na bajaji,kifungu cha 23(7)kinachompa mamlaka mtahini wa udereva kumpitisha dereva kwa amefaulu na hivyo anafaa kupewa leseni na msajili.
''Kifungu hiki hakimwajibishi afisa yeyote wa serikali au mtahini au mtu yeyote aliyejiusisha katika kufanya udanganyifu wa kumtafutia mtu leseni ya usereva ambaye hana sifa za zinazostahili,hivyo sheria na kanuni haziweki bayana sifa ambazo anatakiwa mtahini kuwa nazo huyo anayetakiwa kutahini madereva wanafunzi ,hivyo ifike wakati sasa sheria ikafanyiwa marekebisho ili kuweza kuwaadhibu Maofisa kama hawa''alisema.
Kwa upande ambao unamruhusu sajili kumpa mtu leseni ya udereva kwa kutumia uzoefu wake bila kupitia shule kifungu hiki kwasasa yafaa kirekebishwe kwa kumtaka kila mtu kupita katika shule ya udereva uliyo sajiliwa rasmi kwa ajili ya kufundisha madereva kabla ya kupata leseni.
kwa upande wake mkurugezi msaidizi wa habari na mawasiliano kwa umma kutoka taasisi ya mabalozi wa usalama barabarani (RSA )Ramadhani Msangi aliainisha baadhi ya orodha ya makosa yanayoweza kumfanya mtu afungiwe leseni yake au kufutiwa na (mahakama lazima ifungie au kufuta leseni)kifungu cha 27(1)kinatoa orodaha ya makosa amabayo kwayo leseni inaweza kufungiwa au kufutwa kwa lazima ya mahakama
Amesema kuwa makosa lazima ambayo yanaweza kufutwa leseni kwa muda wa miaka mitatu kwa mujibu wa kifungu cha cha sheria 27(1) dereva anaweza kufutiwa leseni na mahakama,iwapo kwa mara ya kwanza ametenda makosa  kama vile kusababisa madhara ya mwili au kifo kwa njia ya uendeshaji wa hatari,kutokuwa makini barabarani,kuendesha kwa papara au kwa hatari,kuendesha gari dereva huku akiwa amekunywa pombe au ametumia madawa ya kulevya,kuendesha akiwa hana leseni halali au wakati leseni ikiwa imefutwa au kufungiwa
''Dereva anaweza kufungiwa au kufutiwa leseni iwapo atakuwa ametenda makosa ya hatari kwa mara ya kwanza kutokuwa makini barabarani,matumizi mabaya ya gari lake barabarani bila kujali watumiaji wengine wa barabara ,kutokuifanya hai leseni yake na kuondolewa sifa za kuendesha gari''Alisema
Aidha ameyataja makosa mengine kuwa ni sambamba na dereva kufungiwa leseni kwa muda wa miezi sita iwapo kwa mara ya pili ametenda makosa yaleyele ya awali,kufungiwa kuendesha gari kwa muda wamiezi 12 iwapo atakuwa hajatimiza wajibu wake baada ya ajali mfano kusaidia majeruhi wakati ilikuwa salama kufanya hivyo au kutoripoti ajali kwa wakati,
Pia dereva anaweza kufungiwa leseni kutokana na ulevi iwapo atakuwa na kiwanmgo cha ulevi kisichozidi 150mg katika 100mls za damu atafungiwa kuendesha kwa miezi sita na endapo atarudia atafungiwa kwa miaka mitatu,kilevi kilichozidi 150mg atafungiwa kuendesha kwa miaka miwili na endapo atarudia atafungiwa kwa miaka sita.
Amesema mapendekezo katika sehemu hii ni kuondoa kosa la kifungu cha 40:kusababisha madhara kwa mwili au kifo kupitia uendeshaji wa hatari linalojitokeza katika kifungu kidofo cha kwanza cha aya ya a-d ya kifungu cha 27(1)madereva hatari wapewe adhabu kali zaidi wakati wale madereva wazembe wapewe adhabu ya chini kidogo
Aidha inapendekezwa kipengele kuhusu makosa ya ulevi katika kifungu cha 27(1)kifutwe chote ili adhabu zake zibakie katika kifungu cha 44-49 ambapo kinahusu nmakosa yanayohusiana na ulevi,pia wameshuri katika sehemu hiyo yachambuliwe vizuri ili wanaoendesha kwa hatari barabarani bila kujali watu wengine leseni zao zifunguiwe kwa muda mrefu zaidi na katika kipindi ambapo leseni zao  zifungiwe walazimishwe kurudi shule.
Amehitimisha kwa kusema kuwa wanahitaji marekebisho ya sheria ya usalama barabarani kwa kuyapa kipaumbele yanatakiwa ya haraka ni yale ya yanayohusu ulevi,mwendokasi,ufungaji wa mikanda,uvaaji wa kofia ngumu (helmeti) magari madogo,amesema hayo ndiyo mambo ambayo RSA wa kuchagiza marekebisho ya sheria ya usalama barabarani  imeyalenga kwa sasa


MWISHO






Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: