Na Amon Mtega Songea

JESHI la polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukakamata baadhi ya samani mbalimbali za ndani zinazodaiwa kuibiwa kutoka kwenye maeneo (Makazi) ya  raia wema.

 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa amelitaja tukio hilo limetokea Januari mosi hadi saba mwaka huu wakati jeshi hilo lilipoendesha msako .

 Kamanda Maigwa amezitaja samani hizo kuwa ni  Screen za televisheni kumi na moja (11) majiko ya Gesi mawili madogo ambayo ni aina ya Orxy kg,14.5 na Mihan kg .14.5 na vingine kuwa ni Radio Subufa aina ya Sea piano mbili pamoja na spika zake tatu,deki mbili aina ya mr uk,play station tatu aina ya Sonny pamoja na Godoro la tano kwa sita.

 Amevitaja vitu vingine kuwa ving’amuzi vitatu ambapo Star times viwili ,Azam moja na adapter yake ,dishi la Azam moja ,Pikipiki moja rangi nyeusi aina ya Haojue ambayo haina plate namba na vichwa vya Kompyuta viwili aina ya Dell na Lg (CPU)na monita za Kompyuta mbili  aina ya Dell na Hp.

Kufuatia msako wa kuvikamata vitu hivyo kamanda alisema watu tisa wanashikiliwa kwa mahojiano na  upelelezi ukikamilika watayataja majina yao ,huku amewataka wakazi wa mkoa huo kwenda kuvitambua vitu hivyo kama kuna mkazi aliibiwa.

Aidha kamanda huyo amelitaja tukio lingine kuwa la mwanafunzi wa darasa la saba Shaibu Kaisi (18)wa shule ya msingi Mbulani mkazi wa Kipera kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea amefariki dunia kwa kupigwa na radi kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

   Kamanda alifafanua kuwa tukio hilo limetokea Januari sita mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni huko katika maeneo ya Kipera wakati mwanafunzi huo akiwa barabarani karibu na Nyumbani kwao.

                                 MWISHO.
Share To:

Post A Comment: