NA MWANDISHI WETU, BUSEGA

MBUNGE wa Jimbo la Busega, Mkoani Simiyu Dkt. Raphael Chegeni amezindua mradi wa maji kijiji cha Busami uliopo katika Kata ya Badugu kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mradi huo ni pamoja na wa kijiji cha Mwamigongwa Kata ya Malili imeweza kujengwa kwa gharama ya shilingi milioni 568 kwa msaada huo wa UNDP.

Kwa uzinduzi huo kwa sasa wananchi wa maeneo hayo watapata maji safi na salama

"Tuliahidi tunatekeleza; Busega hiyo inasonga mbele.
Sambamba na miradi hii ipo miradi mingine inaendelea kutekelezwa."  Alisema Dkt. Chegeni.

Aidha, katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT) Wilaya ya Busega, Winfreda Kinasa kwa kutambua mchango wa Mbunge wa jimbo hilo wamemtunukia tuzo maalum.

Tuzo hiyo maalum amekabidhiwa Dkt. Chegeni kwa kutambua mchango wake mkubwa kwa akina Mama wa Wilaya na hasa kwa kuwahamasisha kuanzisha miradi pamoja na kuwasaidia kwa hali na mali.

"Kazi unayofanya kwa maendeleo ya wana Busega ni mfano wa kuigwa, tunajivunia kuwa na mbunge Imara, makini na shupavu katika kuleta maendeleo" alisema  huyo Kinasa.


Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: