Na  Ferdinand Shayo,Arusha.



Zaidi ya ekari 3000 zimesimamisha uzalishaji wa shayiri kutokana na wanunuzi wakubwa wa ngano inayozalishwa kata ya Monduli juu kusitisha ghafla mkataba wa kununua mazao yao.





Wakulima wakizungumza katika kikao chao ,wamesema kuwa kusitishwa kwa mkataba wa kampuni ya mnunuzi kutawaathiri wakulima kwani hawana mazao mbadala ya kuotesha kutoka na msimu wa mazao mengine kupita jambo ambalo litawasababishia hasara.



Aidha  Wakulima hao Loretu Leyan na Moloimet Sane wameshangazwa na kitendo cha mnunuzi huyo kuvunja mkataba na wakulima licha ya kuwa mnunuzi mzuri kwa miaka 20 ilitopita na sasa wakulima hawana mbadala.



Hata  hivyo wakulima hao  Langoi Katibu  wameiomba serikali iangalie ie namna mbadala ya kununua mazao yao  ili kuendeleza kilimo cha shayiri na kuwawezesha wakulima.kupata kipato.



Mwenyekiti wa Wakulima hao Sokoine Leyan  amesema.kuwa kusimama kwa uzalishaji wa shayiri kutaathiri kipato cha wakulima na kupelelea kuzorota kwa maendeleo hivyo ameiomba serikali ichukue hatua ili kuwanusuru wakulima.



Afisa Ushirika wa wilaya ya Monduli Ester Tarimo amesema kuwa wakulima wa wilaya za jirani za karatu na mbulu pia wameathirika na mnunuzi huyo kuvunja mkataba.



Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Monduli Salimu Omar , amesema kuwa wamefika na kusikiliza kero za wakulima hao na kuahaidi kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuleta ufumbuzi wa tatizo hilo.


Hata hivyo Wanunuzi hao ambao ni Maafisa wa Kampuni ya Bia ya TBL ,walifika kuzungumza na viongozi katika kikao cha ndani ambacho hawakutaka waandishi wa habari waingie na pia baada ya kumaliza kikao hawakutoa ushirikiano wowote kwa wanahabari kwa maana ya kutokua tayari kuongea.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: