Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo akimtua ndoo ya maji kuonesha mradi wa Maji wa Kisarawe umekamilika na wananchi wa Mji huo kuanza kupata huduma ya maji safi uliojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.


Baada ya kutimiza agizo la Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kupelekea maji katika Mji wa Kisarawe,  Waziri wa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jaffo ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.

Jaffo ametembelea mradi wa maji wa Kisarawe na kuipongeza Dawasa kwa kufanya kazi ya kupelekea maji kwenye mji huo ndani ya muda mfupi.

Amesema kwa mchango mkubwa walioutoa Dawasa katika Mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Pwani ikiwemo Kisarawe ameahidi kuwapatia cheti cha Ubora kutoka Wizara yake.

Jaffo amesema, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja ametekeleza maagizo ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kuleta maji kwenye mji huo baada ya miaka mingi ya kero ya ukosefu wa maji safi.

Amesema, mradi huo umejengwa kwa fedha za ndani za Dawasa ambazo takribani Bilion 10.6 zimewezesha kukamilika kwa  mradi huo na kwa sasa wakazi wa Kisarawe na maeneo ya viwanda wanapata maji.

"Kwa sasa mahitaji ya wananchi wote wa Kisarawe na Viwanda  ni Lita Milioni 1.2 na Dawasa wametuletea maji Lita Milion 6 kwa siku kwa hiyo tuna akiba ya maji Lita Milioni 4.8 tunawashukuru sana,"amesema Jaffo.

"Tumeona mradi huu, ila nauomba uongozi wa Dawasa uangalie na maeneo mengine kuna eneo la Kisanga, Masaki na sehemu zingine kupelekea huduma hii ya maji wananchi wananunua dumu moja kwa shilingi 1000 shida ya maji ni kubwa sana," amesema

"Kuna eneo la Sanze kule watendaji wangu wote wa serikali wanakaa kule nina imani watapata maji ndani ya muda mfupi," 

Mbali na hilo, Jaffo amewataka wananchi kujiunga na huduma ya Maji kwa mkopo ambapo amemuagiza Mtendaji Mkuu kuongeza muda wa mkopo hadi miaka miwili ili kuendana na hali ya kiuchumi ya wananchi.

Naye Mhandisi Luhemeja amemshukuru Waziri Jaffo kwa kuona kazi kubwa waliyoifanya na wamemuahikishia maeneo yote aliyowaelekeza watayafanyia kazi.

Luhemeja amesema, amechukua agizo la kuongeza muda wa mkopo kwa wananchi hadi kufikia miaka miwili na amewataka Watendaji wa Dawasa  Mkoa wa Kihuduma Kisarawe kuanza kuyafanyia kazi.

"Kwa sheria mpya ya mwaka 2019,Kisarawe ni Mkoa wa Kihuduma wa Dawasa kuna baadhi ya maeneo mengine hatujapeleka huduma ila kwa maagizo yako tunafanyia kazi,"

Mradi wa Kisarawe umekamalika mwishoni mwa mwezi Oktoba na tayari  Dawasa wanaendelea kufanya maunganisho mapya   kwa wateja na vizimba vikiendelea kutoa maji.

 Msimamizi wa Mradi wa Maji Kisarawe Mhandisi Ishmael Kakwezi akielezea mradi wa maji wa Kisarawe kwa Waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo kuanzia Tenki la la maji Kibamba hadi Kisarawe.

 Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo akifungua maji kuonesha mradi wa Maji wa Kisarawe umekamilika na wananchi wa Mji huo kuanza kupata huduma ya maji safi uliojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA.

 Afisa Mtendaji Mkuu ws Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuelezea jambo Waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa Maji Kisarawe leo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuelezea jambo Waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa Maji Kisarawe leo.

Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo akiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe kuanzia kwenye tanki la Kibamba ilipofungwa Pampu ya Kusukumia maji (Booster Pump) hadi tanki la Majk la Kisarawe lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni 6 kwa siku.
Share To:

Post A Comment: