Na Elizabeth Ntambala ,Msumbanews Rukwa
MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (pichani )ameziagiza Halmashauri  za mkoa kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 2888 ili wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza waweze kwenda Sekondari.

Agizo hilo alilitoa hivi karibuni  wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa Rukwa(RCC) katika mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi  wa Jengo  la ofisi ya mkuu wa mkoa

Alisema kuwa wanafunzi Waliofaulu darasa la saba mwaka 2019 ni 16,069,kati ya hao wavulana ni 7,953 na Wasichana ni 8,116, na nafasi zilizopo ni 13,128.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Wanafunzi ambao watakosa nafasi katika Halmashauri ya wilaya ya Kalambo ni 361,wilaya ya Nkasi Wanafunzi 1554, wilaya ya Sumbawanga Manispaa ni Wanafunzi 179 na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni Wanafunzi 794.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: