Mratibu wa mradi wa vijana na jinsia (USID Boresha Afya ) Faith Dewasi akielezea kazi za mradi huo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili
Kaimu katibu tawala mkoa wa Iringa Lucas Kambelenje akitoa TAKWIMU za hali halisi ya ukatili wa kijinsia mkoa wa Iringa
Baadhi ya washiriki kutoka asasi mbali mbali wakiwa katika maadhimisho hayo
..................................................................
Wakati takwimu za jeshi la polisi zikieleza kuwa watoto 657 wanawake 414 wanawake 414
na wanaume 41 kwa mwaka huu 2019 mkoa wa Iringa wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ,mradi wa wa jinsia na vijana (USID Boresha Afya ) umepania kuendelea kutoa elimu kwa jamii ya mkoa huo ili kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia .
Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ulimwenguni jana katika maadhimisho ya mkoa yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Kiwere wilaya ya Iringa mratibu wa mradi huo Faith Dewasi alisema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya mkoa wa Iringa vimezidi kusika kasi jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa maendeleo ya kiuchumi katika mkoa huo .
Hivyo alisema pamoja na mradi USAID Boresha afya upande wa jinsia na vijana umeendelea kutoa elimu mbali mbali kwa makundi mbali mbali ili kusaidi kupunguza kama si kumaliza tatizo la ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii ya wakazi wa mkoa wa Iringa na kuwa kazi hiyo imeendelea kuwafikia watu wengi zaidi na sehemu mabadiliko yameanza kuonekana kwa jamii kupaza sauti pale wanapoona vitendo vya ukatili vinafanyika katika maeneo yao .
" Ikumbukwe kuwa tupo katika maadhimisho ya kupinga ukatili duniani na sisi kama shirika ambao tunapata msaada wa fedha kutoka kwa watu wa Marekani tumeweza kufanya kazi kubwa ndani ya mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na ofisi za serikali mkoa wa Iringa kwa kuwafikia wananchi wa makundi mbali mbali wakiwemo walemavu ,walimu ,viongozi wa serikali na makundi mengine ili kufikisha elimu hiyo " alisema
Aidha alisema elimu hiyo imekuwa ikiwafikia wataalam mbali mbali wakiwemo madaktari ,watu maarufu na wengine ili kuonyesha kuwa suala la ukatili wa kijinsia ni la makundi yote na wote wanahitaji kufiiwa na elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia ili kuweza kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii nzima .
Hata hivyo alisema kutokana na elimu ambayo wamepata kuitoa kwenye makundi mbali mbali mbali na mahojiano ambayo wameyafanya kwenye makundi hayo inaonyesha suala la ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Iringa linazungumzwa kwa zaidi ya asilimia 60 hali inayoonyesha kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa elimu ya kupinga ukatili kuendelea kutolewa kwa jamii .
Dewasi alisema mradi huo wa Boresha afya umekuwa ukipiga vita vitendo vya ubakaji katika jamii kwani kumekuwepo na matukio mbali mengi ya ubakaji ,ulawiti na utatili mwingine kwa watoto watoto katika mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa asilimia zaidi ya 80 ya wanawake na watoto ndani ya mkoa wa Iringa wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili huku wanaume ikiwa ni asilimia 10 wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia na wake zao ila wamekuwa wakitunza siri kwa kutosema popote .
Kuwa wanaume wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia ila wamekuwa hawasemi popote kutokana na mila na desturi walizonazo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Iringa ambao wamekuwa wakiamini kwenda dawati la jinsia polisi kulalamika kwa kupigwa na mwanamke kwao ni aibu jambo ambalo si sahihi kwani vitendo vya ukatili wa kijinsia havitakiwi kukumbatiwa kabisa kwa mtu yeyote bila kujali ni mwanamke ama mwanaume anatendewa ukatili .
Alisema kuendelea kukumbatia vitendo vya ukatili ama kuficha siri ya matukio ya ukatili yanapotokea ni kuurudisha nyuma mkoa na Taifa katika suala zima la uzalishaji mali na kupelekea manyanyaso kwa watoto katika familia kwani kama baba na mama wanatabia ya kufanyiana ukatili suala la matunzo kwa watoto huwa la kiwango cha chini zaidi hivyo ni vizuri kila mmoja kupaza sauti na wao kama mradi wa USAID Boresha afya wataendelea kutoa elimu dhidi ya vitendo vya Ukatili wa kijinsia .
Akitoa taarifa ya hali ya ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Iringa kwa niaba ya katibu tawala mkoa Happines Seneda , katibu tawala msaidizi mkoa wa Iringa Lucas Kambelenje alisema kuwa hali ya vitendo vya ukatili katika mkoa wa Iringa inaendelea kuwa kuwa ambapo takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto ,wanawame na wanaume wanaofanyiwa ukatili imezidi kuwa kubwa .
Alisema kwa mwaka 2018 watu waliofanyiwa ukatili na kuripoti polisi ni watoto 406 ,wanawake 430 ,na wanaume 25 wakati mwaka 2019 takwimu ziliongezeka kwa kuwa watoto 657 wanawake 414 na wanaume 41.
Alisema kuwa ukatili umekuwa unafanyika majumbani ,njiani wakati watoto wanakwenda ama kutoka shule na katika kubaliana na tatizo hilo jitihadfa mbali mbali zinafanyika kwa mwaka jana 2018 watuhumiwa 579 walikamatwa na watuhumiwa 659 kwa mwka 2019 walikamatwa kati yao watuhumiwa 64walitiwa hatiani mwaka 2018 na mwaka 2019 watuhumiwa 25 walitiwa hatiani kwa kukutwa na makosa ya kufanya vitendo mbali mbali vya ukatili wa kijinsia .
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ambae aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela katika maadhimisho hayo aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili sheria
iweze kuchukua mkondo wake .
iweze kuchukua mkondo wake .
Alisema kuwa kwa upande wa wilaya ya Iringa umeanzisha ushirikiano wa jeshi la zima moto na uokoaji kwa kutumia namba ya zimamoto 114 kwa wananchi kupiga simu bure ili kufichua matukio ya ukatili yanayofanyika katika maeneo yao .
Post A Comment: