Monday, 2 December 2019

NAIBU WAZIRI SHONZA AWATAKA MAAFISA HABARI WA SERIKALI KUONGEZA UJUZI KATIKA MAENEO YA KAZI ILI KWENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIANa.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo  Mhe. Juliana Shonza amewataka Maafisa Habari wa Serikali kuongeza zaidi katika ujuzi  wa Taaluma yao kwenye maeneo ya kazi ili kwendana na kasi ya Mabadiliko ya Sayansi na teknolojia.

Naibu Waziri Shonza amesema hay oleo Disemba 2,2019 jijini Dodoma katika ufunguzi wa semina elekezi ya kuwajengea Uwezo Maafisa Habari wa Serikali  ijulikanayo kama ”STRATEGIC WRITING SKILLS FOR GOVERNMENT COMMUNICATORS “ inayoratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali.

 Mhe.Shonza amesema ili kuweza kuwa na Wanahabari Mahiri ni lazima pawe na ujuzi hivyo huwa anasikitishwa kuona vyombo vya habari Binafsi vinafanya vizuri kuisemea serikali kuliko vya serikali hivyo kuna haja kubwa ya kuongeza kasi ya utendaji kazi kwa ueledi kwa maafisa habari wa Serikalini.

“ili kuweza kuwa na wanahabari magwiji lazima pawe na ujuzi,haiwezekani sayansi na teknolojia inabadilika na ujuzi unabaki palepale.Mafunzo mtakayopata yawe chachu kwa maendeleo ya taifa letu.Watanzania kwa sasa wamekuwa makini  kufuatilia namna serikali inavyofanya kazi na wanaotoa hizo taarifa ni ninyi wanahabari”amesema.

Aidha ameongeza “Ninyi ndio injini ya serikali na vinara na kuna umuhimu sana wa kuisemea serikali na inanisikitisha waandishi wa au vyombo vya habari binafsi vinafanya kazi vizuri kuliko ninyi,na wakati huwa ninawashangaa wanahabari kwenye  page ya Wizara unakuta ina followers 20 wakati mwingine huwa ninawauliza watu 20 habari za wizara unazopata wapi watu wa kuzisoma taarifa wakati una wafuasi wachache.”Katika hatua nyingine Mhe.Shonza amewataka Maafisa habari wa Serikali kutilia mkazo katika matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii kwani ndio  njia  pekee na ya haraka inayofikisha ujumbe wa Serikali kwa Watanzania.

“Asikwambie mtu sasa hivi mitandao ya kijamii ndio inayofuatiliwa zaidi kwa sasa ,mtu hasubiri gazeti muda huohuo tukio linapotokea anafuatilia kwa Maafisa habari wa serikali msiibeze mitandao ya kijamii mfano facebook,twitter,Instragram,Blogs kwa dunia ya leo zimeshika kasi mno katika sekta ya habari,mtu yuko radhi alale njaa lakini anunue bundle ajue nini kinajiri.”amesema.

Kwa upande wake Msemaji mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa Idara  ya Habari Maelezo Dokta Hassan Abbas amesema katika semina hiyo wapo wataalam mbalimbali watakaotoa semina elekezi huku Mada mbalimbali zitatolewa na Wataalam hao pamoja na kupeana uzoefu katika sekta ya Habari.

Semina Elekezi kwa Maafisa habari wa Serikali itatumudu kwa muda wa siku tano kuanzia Disemba 2 hadi 6,2019 ambapo  watajadili namna ya kuripoti kwa usahihi Habari za Serikali pia jinsi ya kuwahabarisha Watanzania Miradi mbalimbali mizuri ya Maendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya Tano.
No comments:

Post a comment