Sunday, 29 December 2019

Mbunge wa Arumeru Mashariki Awataka WanaCCM kushikamanaNa Ferdinand Shayo,Arusha.

Mbunge wa Arumeru Mashariki John Pallangyo amewataka wanachama wa CCM  wa jimbo hilo kushikamana na kulinda mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake ikiwemo ukarabati wa barabara za vijijini ambazo zilikua hazipitiki kwa miaka mingi pamoja na kutatua kero za wananchi.

Akizungumza katika semina elekezi kwa wenyeviti wa vijiji juu ya uendeshaji wa serikali za mitaa ambapo amewapongeza Makada wa chama hicho waliomuunga mkono na katika heka heka za uchaguzi ndani ya chama hicho na kufanikiwa kupita bila kupingwa .

John amesema kuwa Wanaccm wanapaswa kudumisha umoja na mshikamano na kushirikiana na viongozi wa serikali katika kusukuma gurudumu LA maendeleo katika jimbo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amesema kuwa licha ya kipindi kifupi cha Mbunge huyo amefanikiwa kukarabati barabara za vijijini ambazo kwa miaka mingi zilikua hazipitika na kusababisha adha kwa wananchi.

Muro amesema kuwa ataendelea kumuunga mkono Mbunge huyo katika kufanikisha adhma ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea Maendeleo kwani jukumu LA msingi alilonalo ni kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

No comments:

Post a comment