Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Dkt.Balozi Ali Idd akizungumza katika Kongamano la tatu la Kiswahili la Kimataifa lililoandaliwa na Baraza la kiswahili la Zanzibar  ambapo amemuwakilisha Rasmi ni Mhe.Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi 

 Waziri wa vijana Utamaduni na Balozi ALI Karume Waziri wa Vijana Tamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar akizungumza na washiriki wa kongamano la tatu la Kiswahili Zanzibar BAKIZA

Washiriki wa Kongamano la tatu la Kimataifa Kiswahili linaloendelea katika ukumbi wa Sheikhe Idris Abdul Wakil Mnazi mmoja Zanzibar 
Washiriki wa Kongamano la tatu la Kimataifa Kiswahili linaloendelea katika ukumbi wa Sheikhe Idris Abdul Wakil Mnazi mmoja Zanzibar
Kongamano likiendelea katika ukumbi wa mikutano wa heikh Idris Abdul Wakil Mnazi Mmoja Zanzibar


Na.Vero Ignatus,Zanzibar

Kongamano la tatu la Kiswahili la Kimataifa lililoandaliwa na Baraza la kiswahili la Zanzibar limeanza leo ambapo mgeni Rasmi ni Mhe.Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye amewakilishwa na makamu wa pili wa rais Zanzibar  Mohamed Seif  Khatib.

 Rais Zanzibar Dkt.Ally Mohamed Shein amelipongeza Baraza hilo kwa kuandaa kongamano la kimataifa linalowakusanya wataalam mbalimbali wa kiswahili duniani.

Shein amesema Watanzania wanatakiwa kuitumia lugha ya kiswahili  kwenye majukwaa mbalimbali ya Kitaifa na kimataifa ili kuonyesha uzalendo na kuendeleza kukuza lugha na kukitukuza kiswahili.

Akizungumza kwa niaba yake Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Dkt.Balozi Ali Idd amesema kuwa kongamano hilo ni muhimu kuendelezwa kwasababu linatoa fursa mbalimbali kwa wataalamu wa changa wa luha ya kiswahili kuchangamana na wenzao wakongwe bila ubaguzi wowote ule.

Dkt.Ali Idd amesema ni vyema wataalam wa lugha ya kiswahili wakaandika maandiko yenye tija na yenye kujikita kwenye fasihi na Isimu  ili ziweze kuelezeka vyema katika jamii na kuthamini umuhimu wa kuenea kwa lugha ya kiswahili katika bara la Afrika na ughaibuni ili kuhakikisha kuwa lugha ya kiswahili inatumika kwa ufasaha .

''Zichangamkieni na kuzitafutia fursa za lugha  hii ya kiswahili katika Muungano wetu na katika nchi mbalimbali ili kuikuza lugha hii ya kiswahili kwasababu hali ya lugha ya kiswahili duniani kwa sasa ni bidhaa adhimu inauzika katika soko la ndani na nje ya nchi''alisema

Amesema lugha ya kiswahili haijatokea kwa bahati mbaya bali ni juhudi mbalimbali zilizotumika ili kuweza kuwa utambulisho wa Afrika,amesema kinachohitajika ni kuwa na mipango imara ya kuzitumia fursa hizo za lugha ya kiswahili.

Amesema jukumu la Baraza la Kiswahili Zanzibar  (BAKIZA )ni kuwaonyesha na kuzitafuta fursa za kiswahili popote zilipo duniani na kuanza kuzitumia kwani ni bidhaa adhimu.

Kwa upande wake Waziri wa vijana Utamaduni na Balozi ALI Karume Waziri wa Vijana Tamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Magufili kwa ushawishi wake kwa viongozi wenzake 14 wa Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC )Kwamba Kishwahili kitumike kama lugha rasmi 

Amesema kongamano hilo ni fursa kwa washiriki kujadili fursa mbalimbali za Kiswahili duniani hivyovijana wanaosoma lugha ya kiswahili wanapaswa kuzichangamkia fursa hizo 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la kiswahili la (BAKIZA )Dkt.Mohamed Seif Khatib amesema kuwaidadi ya washiriki wa kongamano imeongezeka kutoka 147 mwaka 2017 hadi kufikia 270 mwaka huu

Awali alisema kuwa washiriki walikuwa 147 mwaka 2017,237( 2018)na 270 kwa mwaka 2019 amabapo kwa kongamano hilo litakuwa fursa ya kumkabidhi Rais wa Zanzibar Dkt.Shein kazi za Kitaalam (Tasnifu)zilizofanywa na wataalamu mbalimbali katika ngazi ya uzamili (Masters)na Uzamivu( PHD)

Aidha  Kongamano hilo la tatu la Kimataifa limebeba kauli mbiu isemayo Fursa za soko la kiswahili duniani katika maendelep ya Fasihi na Isimo

Mwisho


Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: