Wednesday, 18 December 2019

ILALA YATAKIWA KUWEKA MKAKATI JUU YA LISHE

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Nicodemus  Shirima akizungumza katika Mafunzo ya  mipango bajeti ya kutekeleza Afua za Lishe Manispaa ya Ilala 
Baadhi ya washiriki katika Mafunzo ya  mipango bajeti ya kutekeleza Afua za Lishe Manispaa ya Ilala
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dar ES Salaam Hamis Ngoda akizungumza katika mafunzo ya mipango bajeti ya kutekeleza Afua za lishe Manispaa ya Ilala 

Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shaibu akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi wa Ilala katika mifunzo ya mipango bajeti   ya Afua za lishe Manispaa ya Ilala NA HERI SHAABAN
HALMASHAURI ya Ilala yatakiwa kufanya vizuri katika kutekelezaafua mbalimbali za lishe kadiri mipango na bajeti ya lishe ili halmashauri zingine zifanye vizuri.

Ushauri huo umetolewa Manispaa ya Ilala jana na Hamis Ngoda  aliyemwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam katika mafunzo ya maandalizi ya  Mipango na bajeti ya lishe.

" Dar ES Salaam inatokana na Wilaya ya Ilala ,ambayo ikifanya vizuri katika bajeti wilaya zingine zitafanya vizuri na mkoa wetu utakuwa wa kwanza katika kuepuka tatizo la utapia mlo" alisema Ngoda .

Ngoda alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala  kusimamia masuala ya lishe hasa katika ngazi ya jamii kadiri ya vipaumbele vya lishe.


Aidha alisema kila mjumbe  wa Kamati ya Lishe ya Manispaa akitimiza wajibu wake  changamoto ya lishe duni itakwisha.

Aliagiza vikao vya Kamati ya Lishe vifanyike kwa kuzingatia kanuni na kalenda ya vikao vya Halmashauri.

Aliagiza watoa huduma  vituo vya kutolea huduma za afya na ngazi ya jamii wawezeshwe ili kutoa elimu ya kutosha kwa walengwa hasa akinamama wajawazito , wanawake wanaonyonyesha,watoto wachanga na wadogo ili wapate elimu ya lishe bora na kuepuka matatizo yanayoweza kusababishwa na lishe duni.

Kwa upande wake mgeni rasmi Nicodemus Shirima ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala  alisema katika kuelekea uchumi wa viwanda jamii ya Watanzania inaendelea kuathirika na changamoto mbalimbali za lishe hasa kwa watoto chini ya miaka mitano.

Shirima alisema lishe duni inayoathiri ukuaji wa mwili na Maendeleo ya mtoto lakini pia inathiri Maendeleo yake kiakili na uwajibikaji wake katika kipindi cha utu uzima .


Naye Afisa Lishe Manispaa ya Ilala Flora Mgimba alisema dhumuni la mafunzo hayo ni kufanya maandalizi ya awali ya mpango na bajeti ya  jumuishi ya lishe kwa mwaka wa fedha 2020/2021.


Meya   wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto alisema kama Halmashauri watahakikisha elimu ya lishe bora inafika kwa jamii il kukabiliana na tatizo la utapia mlo.

No comments:

Post a comment