Friday, 27 December 2019

ASKOFU DALLU AWATAKA WATUMISHI KUSHINDA VISHAWISHI


                       


Na Amon Mtega,Songea

  ASKOFU Mkuu wa  Kanisa la Romani Katoliki Jimbo kuu la Songea ,Damian Denisi Dallu amewataka Watumishi  wa Kanisa hilo kushinda vishawishi vilivyopo Ulimwenguni ili kuendelea kuwa mfano bora mbele ya jamii wanazozihudumia Kiroho na Kimwili.

 Wito huo ameutoa jana wakati akihubiri kwenye Misa ya kumuweka daraja Takatifu la Ushemasi, kwa Shemasi Nelson Ngonyani iliyofanyika jimboni hapo kwenye Kanisa la Mtakatifu Mathias Mlumba Kalemba lililopo mjini Songea.

 Askofu Dallu akihubiri kwenye misa hiyo amsema kuwa kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya watumishi wa Mungu wanaohudumu kwenye makanisa kuingiliwa na vishawishi vya Ulimwengu jambo ambalo hupelekea jamii kushindwa kuwaelewa watumishi hao.

 Amesema kuwa kazi ya utumishi wa Mungu ni kutoa huduma hivyo inapaswa ifanywe kwa unyenyekevu na kuzingatia maadili pamoja na viapo vya Mungu vilivyowekwa ambavyo vitashinda vishawishi.

 “Ulimwengu wa sasa vishawishi vya mambo mabaya vinawaingia watumishi wa Mungu hadi makanisani na Nje ya makanisa hivyo ni vema kuvishinda vishawishi hivyo kwa kumuomba Mungu”amesema Askofu Dallu.

   Aidha amesema kuwa katika muendelezo wa sikuku za kuzaliwa kwa Yesu Kristo yawapasa watumishi hao kujitafakari na kutambua wapi wanakosea ili warudi kwenye misingi inayotakiwa na Mungu .

 Kwa upande wake Shemasi Nelson Ngonyani wakati akipata kiapo cha daraja hilo mbele ya Askofu huyo na waumini wa kanisa hilo amesema kuwa atayatimiza yote kwa msaada wa Mungu .

   Shemasi Nelson Ngonyani anatokea Jumuiya ya Mtakatifu Marko Kingango cha Mshangano Porokia ya Tanga Jimbo kuu la Songea lililopo mkoani Ruvuma

No comments:

Post a comment