Watanzania na wanachama wa chama cha Mapinduzi ( CCM ) kupitia Tawi la CCM Nchini  China chini ya Katibu wa Tawi, Ndugu Yazid Iddi walipata mwaliko wa kukutana na Katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) Mwalimu Raymond Mangwala katika ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Jiji Dodoma lengo likiwa kushauriana kama Vijana namna kuendelea kukisimamia Chama Cha Mapinduzi.

Katibu wa Tawi la CCM China ndugu Yazid Iddi alitoa salamu za pongezi kwa niaba ya Mwenyekiti wake ndugu Salum Ramia na viongozi na wanachama wenzake wote kwa juhudi za dhati wanazofanya Mwenyekiti wa UVCCM ndugu Kheri James, Makamo mwenyekiti wa UVCCM ndugu Tabia Mwita, Katibu Mkuu wa UVCCM ndugu Mwalimu Raymond Mangwala, na Manaibu katibu wote UVCCM bara na Zanzibar alisema, "Viongozi wa Umoja wa Vijana wamekuwa nguzo imara ndani ya CCM  kwa kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kushika Dola na Kuimarika siku hadi siku kwa kuanzisha program mbalimbali mpya ndani ya Chama kama ile ya "TANZANIA YA KIJANI" Iliyojenga Hamasa kubwa sana ndani ya Chama na kukirahisishia Chama katika Chaguzi zijazo za serikali ya mitaa na uchaguzi Mkuu"

Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndugu mwalimu Raymond Mangwala alisema ipo haja sasa kuanzisha forum zitakazokuwa zinatuunganisha kwa pamoja kama wanaCCM waliopo nje ya nchi na wale waliomo ndani kwa maana ya wanachama na Viongozi kuwa kwapamoja" aliendelea kushauri kuanzishwe umoja wa vijana wa CCM nje ya nchi ambapo kwa kuanzia ni vyema Tawi la CCM China likawa moja ya matawi ambalo program hiyo ianzie kwa lengo la kuendelea kuwaweka Vijana wote pamoja ndani na nje ya nchi"

UMOJA NI USHINDI.

Imetolewa na
Abdul waheed Sarbouk
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Tawi la China
Share To:

msumbanews

Post A Comment: