Friday, 8 November 2019

Vyama 11 vya upinzani vyatangaza kushiriki uchaguzi Serikali za mitaa 2019

Kiongozi wa Vyama 11 vya Siasa visivyokuwa na uwakilishi Bungeni, Abdul Mluya amesema hawawezi kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kama Vyama vingine kwasababu 'mwenye Njaa hawezi Kususia chakula'.

Vyama hivyo ni  DP, SAU,NRA,ADC, UDP,UMD,CCK,TADEA, DEMOKRASIA MAKINI, TLP,AAFP.

Vimetangaza uamuzi huo leo Ijumaa Novemba 8, 2019 jijini Dar es Salaam siku moja baada ya Chadema na ACT Wazalenfo  kujitoa kushiriki uchaguzi huo .

Vimesema vitashiriki vikiamini Wizara ya Tamisemi inayosimamia uchaguzi huo itatenda haki kwa kuwarejesha wagombea wake walioenguliwa kushiriki uchaguzi huo.

“Tunaamini watarudishwa kwa sababu wamekidhi matakwa. Tunataka tushindane kwa hoja na sera kwenye mikutano ya hadhara,” amesema katibu  mkuu wa DP,  Abdul Mluya kwa niaba ya viongozi wa vyama hivyo.

No comments:

Post a Comment