Na Ferdinand Shayo,Killimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Killimanjaro Dr.Anna Mghwira amewataka Wahitimu wa chuo cha ufundi  cha Papa Bridge Vocational Training center kuwa wabunifu na kujiajiri kwa kujiunga pamoja na kuanzisha shughuli za uzalishaji pamoja na kutumia fursa za mikopo zilizoko katika Halmashauri  na taasisi za kifedha badala ya kusubiri kuajiriwa.

Mgwira amesema kuwa umoja wa wanachuo walihitimu ni nguzo muhimu itakayowawezesha kukopesheka na kuaminika kwa urahisi kuliko mtu mmoja mmoja hivyo wanapaswa kujiunga katika vikundi.

Aidha ameahidi kuwaunga mkono wahitimu watakao kuwa mawazo mazuri ya miradi kwa kuwaunganisha na taasisi muhimu ili waweze kupata wanachokitaka .

“Nimefurahi kuona ujuzi unaotolewa hapa ni wa hali ya juu mnapoenda mitaani msiwe wanyonge  tumieni maarifa mliyopata kuleta mabadiliko katika maisha yenu na jamii kwa ujumla” Alisema Mghwira

Muasisi na Mkurugenzi wa Chuo hicho Father,Dr.Aidan Msafiri amesema kuwa chuo hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwakomboa vijana waishio vijijini ambao hawakua na maarifa na ujuzi zaidi ya kukimbilia mijini hivyo kimewasaidia kujikomboa kiuchumi na kifikra.

Aidha amesema kuwa chuo hicho kilianzishwa kwa msaada wa watu wa Australia ambao wamekifadhili cho hicho na kinatoa elimu kwa wanafunzi wote hususan wale wasiokua na uwezo wa kifedha.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: