Waziri wa Maji Profesa Makame Mbara ameanzisha na kufuta Baadhi ya  Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira Nchini ambapo mamlaka  36 zimefutwa  na  maeneo yake yatahudumiwa na mamlaka za makao makuu ya Mikoa.

Akitoa taarifa kwa umma kupitia Vyombo vya Habari, kuhusu muundo mpya wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira Nchini, Katibu Mkuu Wizara  ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa mamlaka zilizofutwa ni pamoja na Usa River,Monduli,Longido,Chamwino,Kongwa na hapa anafafanua zaidi.
Sambamba na hayo amesema kuwa kutakuwa na  mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira 25 katika ngazi ya makao makuu/miji  mikuu ya mikoa pamoja na kuhudumia halmashauri zilizopo katika miji mikuu/makao makuu ya mikoa husika,baadhi ya mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira .

Katika hatua nyingine amesema kutakuwa na mamlaka nane (8) za miradi ya kitaifa na mamlaka 32 katika ngazi ya makao makuu ya wilaya na miji midogo ambapo itaendeshwa na RUWASA katika wilaya husika.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Antony Damian Sanga amesema kuwa amemshukuru Mh Waziri kwa kuendelea kufanya mabadiliko katika wizara ya maji kwani lengo kubwa ni kufanya mabadiliko ambayo ambayo yanawapelekea wananchi kuweza kupata huduma bora yamaji.


Hatahivyo, Profesa kitila amesema  kuwa katika kuimarisha undeshaji wa sekta ya usambazaji wa maji na usafi wa mazingira mijini  Waziri wa Maji Profesa Makame Mbara kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa sheria ya huduma za maji safi na usafi wa mazingira Na.5 ya mwaka 2019,ameongeza maeneo ya huduma kwa baadhi ya mamlaka za maji safi na mazingira nchini, hivyo taarifa hiyo inainisha mamlaka zilizoongezewa maeneo ya huduma,mamlaka mpya zilizoanzishwa na mamlaka zilizofutwa.



Share To:

msumbanews

Post A Comment: