Aliyekuwa mstaiki meya wa jiji la Arusha na diwani wa kat ya sokoni one kupitia chama cha demikrasia na maendeleo(chadema)Bw Kalisti Lazaro amesema kuwa alikuwa anapita  wakati mgumu sana hasa pale ambapo chama hicho kilipokuwa kinamtaka ahirishe vikao au kususa vikao vya mabaraza ya madiwani  kwa ajili ya maslahi  binafsi ya chama hicho alichoondoka.

Pia mbali na kulazimishwa kususa au kuhairisha vikao vya mabaraza ya halmashauri alikuwa analazimishwa kufanya mambo ambayo wakati mwingine yalikuwa yanauweka uzalendo wa taifa mahali pabaya sana
Kalisti aliyasema hayo mapema leo mara baada ya kukabidhi ofisi na kuwaaga  watumishi  wa halmaahauri ya jiji la arusha ikiwa ni siku chache  baada ya kujivya nyadhifa zake zote ndani ya chadema na kujiunga na chama cha mapinduzi (Ccm)

Alidai kuwa amekuwa akipitia wakati mgumu sana kwa kuwa alikuwa anatakiwa afanye mambo ambayo yalikuwa kinyume na uzalendo lakini kamwe hakurudi nyuma alitanguliza uzalendo huu

"Nimekuwa kama meya wa jiji hili kwa kipindi cha miaka kama minne hivi kipindi naingia hapa watu walifikiria sana namna ambavyo kutakuwa na fujo nyingi sana lakini kamwe sikukibali bali nilitanguliza uzalendo mbele japo nilikuwa nikipokea matamko mbalimbali" aliongeza
Katika hatua nyingine alidai kuwa anatamani kuona kilichokuwa chama chake cha awali kikimtakia kila laheri kwa kuwa hatamani kuacha siasa kabisa na anatarajia ataacha siasa pindi atakapofariki dunia

"Chadema wanatakiwa kuniombea kila laheri na pia nikishindwa hata siasa natarajia kufungua kanisa na nitaomba mje kama waumini kwani bado inawezekana kabisa hata siasa zikaendelea huko" aliongeza Kalisti
Hataivyo alimshukuru mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt Maulidi madeni kwa kuweza kumshawishi hadi kufikia hatua ya kujiunga na Ccm na alishawishika baada ya kuona mazuri ambayo yanatanguliza uzalendo mbele 

Naye mkurugenzi wa halmashauri wa jiji la Arusha Dkt Maulid Madeni alisema kuwa kwa mara ya kwanza ameanza kazi ya ukurugenzi akiwa na meya huyo na amemfanikisha sana katika kuboresha kazi za jiji
Dkt madeni alidai kuwa akiwa kama mkurugenzi ambaye yupo karibu sana na meya huyo waliweza kufanikisha miradi mbalimbali ya jiji la arusha na hata kufikia katika ngazi ya taifa

"Kwenye elimu,afya,mazingira,meya bora tumepata tuzo zote hizo ni kwa sababu huyu meya alifanya kazi kwa karibu sana na sisi na hakutupa vikwazo vya aina yoyote ile tunamshukuru sana na tutamkumbuka kwa hali na mali" aliongeza Dkt Madeni.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: