NA HERI SHAABAN
MBUNGE wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Angelina Malembeka (CCM) kesho anatarajia kutoa mafunzo bure ya Ujasiriamali  kwa Wanawake na Vijana wa Mkoa huo.


Akizungumza na waandishi wa habari Bungeni Dodoma leo alisema mafunzo hayo yatakayofanyika kesho ni kwa ajili ya makundi ya wanawake na vijana .

" Mafunzo haya ni endelevu kwa wanawake na vijana kuwapa ili mafunzo kila wakati kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili  kuwakwamua kiuchumi waache maisha tegemezi yameandaliwa na Ofisi yangu " alisema Malembeka.

Malembeka alisema  mafunzo yatakayotolewa kesho katika ukumbi wa Mahonda Zanzibar Sabuni za unga, sabuni za maji, dawa ya kuondoa madoa, dawa ya kusafisha madirisha ya vioo, sabuni ya nywele (shampoo) na vifungashio mbadala .

Awali Mhe. Malembeka alishatoa elimu kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja jinsi ya utengezaji wa Chaki , mishumaa, batik, vikoi elimu ya mikopo na elimu ya ujasiriamali, aidha amewakabidhi mashine za kutengezea chaki tatu, mashine nne za kutengeneza matofali na mashine kumi za kutengeza mishumaa zote amewawezesha  Wanawake na vijana .

Pia alitoa vitanda 10 vya kisasa vya kujifungulia katika  hospital zilizopo  Mkoa wa Kaskazini Unguja


"Katika Majimbo la Mkoa Kaskazini Unguja tayari nimewaunganisha Wanawake na Vijana kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya Tano John Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda na Kauli mbiu yetu "*Mkoa wangu Kiwanda changu"* alisema.

MWISHO
Share To:

msumbanews

Post A Comment: