Friday, 8 November 2019

Mbunge Awatetea wahudumu wa ATCL
Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amelaani kauli iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Kusini, Hasna Mwilima, iliyokuwa ikiwakashfu wahudumu wa Ndege za ATCL kuwa hawana mvuto kwa kuwa kauli hiyo ni ya kejeli na ina mlengo wa kuwadhalilisha wanawake wote.
Mbunge Lema ameyasema hayo leo Novemba 7, 2019, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo ameonesha kukerwa na kauli ya Mbunge mwenzake, aliyoitoea jana Novemba 7, 2019, bungeni Dodoma.
"Kauli ya Mbunge CCM kuwa wafanyakazi wa ndege ATCL (air hostess)hawana mvuto,ni kauli chafu yenye matusi na kejeli kwa wanawake wote,mvuto unatazamwa kwa mambo mengi ikiwa zaidi nidhamu,lugha nzuri,upendo na utaalamu katika huduma, kwani Beauty is in the eye of the beholder" ameandika Lema.
Kwa mujibu wa kauli yake aliyoitoa Mbunge Mwilima, alihoji kuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), hutumia vigezo gani kuwaajiri wahudumu wa ndege hizo.
"Nataka nitanie kidogo, hizi ndege zetu ni nzuri, zinafanya kazi nzuri lakini mle ndani tunapoajiri wale wahudumu, hebu tuangalie wahudumu ambao hata wakiitwa mle kwenye ndege akigeuka hivi hata abiria anaona kweli tunawahudumu, sijui mnatumia vigezo gani, unakuta mhudumu mfupi, hana mvuto wa kuifanya ndege yetu ionekane" alihoji Mbunge Mwilima.

No comments:

Post a comment