Friday, 15 November 2019

Katibu Mkuu CCM awakumbusha Wasanii mambo matatuKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amewataka wasanii kumuenzi hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo kwa kuyaenzi mambo matatu ikiwamo Muungano.

Akizungumza katika kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na wasanii jijini Dar es Salaam leo, ameyataja mambo mengine kuwa ni lugha ya Kiswahili na Azimio la Arusha.

“Napenda niwakumbushe mambo matatu muhimu kwa wasanii la kwanza ni Muungano wetu na wasanii wana mchango mkubwa katika hilo kujifunza na kuielewa historia na kuasisiwa kwake, kuudumisha na kuulinda, la pili lugha ya Kiswahili kukuza na kuilinda na katika hili tunafanya vizuri nimpongeze waziri."

“La tatu ni Azimio la Arusha hili sasa kwa sababu liliweka misingi ya usawa haki na kutukumbusha kuwa sisi hatuna wajomba na tunapaswa kujitegemea kama mnamkumbuka mwalimu mnapaswa pia kuyakumbuka haya muungano, na utaifa wetu.

“Naleta salamu za mwenyekiti wetu wa chama, salamu ambazo ananipa kila mara ninapokuwa kwenye shughuli za siasa anasema anawapenda sana hatawaangusha endeleeni kumuombea na kuliombea taifa.

No comments:

Post a comment