Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Diwani wa kata ya Olasiti Alex Martin  ameitaka serikali kukomesha vitendo vya mauaji na ubakaji katika kata hiyo vilivyoshamiri na kuwa tishio hasa kwa kinamama na watoto wa kike ambao wamekua wahanga wa matukio hayo ambayo yamekua yakijitokeza mara kwa mara.

Akizungumza katika ziara ya Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo aliyetembelea  katika shule ya sekondari Mrisho Gambo ambapo  alikagua ujenzi unaondelea na  kuzungumza na wananchi ,Diwani huyo ameiomba serikali iweze kutumia vyombo vyake vya ulinzi kukomesha mauaji hayo.

Alex ameiomba serikali ijenge kituo kidogo cha polisi kitakachosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa raia kwani eneo hilo halina kituo cha polisi hivyo suala la ulinzi wa watu linakua gumu.

Mkuu wa mkoa Mrisho mashaka gambo  akijibu hoja ya Diwani huyo,ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Mkoa  kufika katika kata olasiti na kushughulikia tatizo la mauwaji kwa kina mama na watoto pamoja na viteno vya ubakaji ili kutokomeza vitendo hivyo na kurejesha hali ya usalama.

Ametoa agizo Hilo katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili ya ukaguzi wa maendeleo ya jiji la Arusha katika ukaguzi wa mradi wa elimu shule ya secondari buruka  iliyopo kata ya olasiti Na kupokea jumla ya madawati  na  viti  zaidi ya 170 kutoka katika taasisi ya kifedha ya NMB Kanda ya kasikazini pamoja na mifuko Hamsini ya simenti kwajili ya ujenzi wa shule hiyo kutoka kanisa la EAGT mkoani Arusha.

Gambo amesema kuwa tukio la kinamama na watoto kuuliwa na kubakwa linasikitisha kwani serikali haiwezi kuvumilia kuona matukio hayo yakiendelea huku kukiwa na watu wanaokisiwa kufanya matukio hayo ambapo ameitaka kamati ya ulinzi na usalama mkoa huo kufanyia uchanguzi na kushuhurikia swala hilo.


Kwa upande wao Wananchi Zainab Kasanga na Joseph Simon  wa kata hiyo wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kushukuru ujio wa Mkuu wa Mkoa ambao unaweza kuwa suluhu kwa changamoto hiyo ya matukio ya ubakaji na mauaji ambao yamekua yakitikisa kata hiyo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: