NA HERI SHAABAN MOROGORO

MKUU wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo ameitaka idara ya Ardhi ya Manispaa ya Morogoro kutatua migogoro yote ya ardhi iliyopo katika wilaya hiyo ili kuwatendea haki wananchi .

Mkuu wa Wilaya Regina aliyasema hayo leo Manispaa ya  Morogoro, wakati wa kuzindua siku maalum ya kupokea kero za wilaya hiyo zikiwemo za migogoro ya ardhi.


"Katika siku ya leo wilaya ya Morogoro tumezindua mpango endelevu kwa mwezi mara moja kwa ajili ya kupokea kero mbalimbali katika uzinduzi huu malalamiko makubwa wananchi wameelekeza kilio chao katika  ardhi  viwanja vyao kuingiliana  kiwanja kimoja kumilikiwa na watu wawili ili tatizo katika wilaya yangu naomba Afisa ardhi limalizike kwa wakati"alisema Regina

Regina alisema dhumuni la kikao hicho cha kupokea kero za wananchi moja kwa moja  ambao wanashindwa kuwasilisha ofisini   kila Jumatano siku ambayo ametenga  kuwasikiliza wananchi Ofisini kwake.

Aidha Regina alisema  halmashauri ya Mvuha Morogoro Vijijini mpango wa kupokea kero utazinduliwa katikati ya mwezi huu.

Awali mwanachi Juma Msafiri  Mkazi wa Kihonda Chuo Cha Kiislam Block 50 alilalamika mbele ya Mkuu wa Wilaya mwanchi Ediga Balaigwa Block 52 amevamia eneo la Block  G 50  ambapo mkuu wa wilaya ameagiza wataalam wa ardhi wakafatilie aliyejenga kwa mwezake avunjiwe.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya Regina Chonjo amewapa siku nne Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)kuweka service line kwa mwananchi Christina Lukwalo mkazi wa Kitungwa eneo la Kingolwila Manispaa ya Morogoro aliyelipa shilingi milioni 3.4 toka mwaka juzi hadi leo ajavutiwa umeme.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheila Edward alimpongeza Mkuu wa Wilaya kwa kubuni mkakati wa kusikiliza kero za wananchi .

Mkurugenzi Sheila alisema  katika halmashauri hiyo wamejipanga na Mkuu wa wilaya Morogoro pamoja na wakuu wa Idara wa halmashauri katika kushirikiana kutatua kero za wananchi.

"Mimi na Watendaji wangu wa halmashauri tupo kwa ajili ya kumsaidia Rais wa awamu ya tano John Magufuli   katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda kutatua kero za wananchi na kuibua miradi ya maendeleo"alisema Sheila


MWISHO
Kikao cha wananchi Manispaa ya Morogoro leo Novemba
07/2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: