Saturday, 23 November 2019

Chuo Cha Uhasibu Arusha(IAA)kimetoa mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa fedha za elimu bure


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA) kimetoa mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa fedha za elimu bure kwa   Wakuu wa shule za sekondari kutoka Halmashauri ya jiji LA Arusha na wilaya ya Arusha ili  kuimarisha usimamizi wa fedha za elimu bure na kujiepusha na matumizi mabaya ya fedha hizo ili ziweze kutumika kuboresha elimu na kuinua kiwango cha ufaulu

Akifungua Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa fedha za elimu bure yaliyotolewa na Chuo cha Uhasibu Arusha,Mkurugenzi wa Haashauri ya Wilaya ya Arusha Advera Ndebagayo amesema mafunzo hayo yatasaidia walimu wakuu kusimamia matumizi sahihi ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya elimu bure na pia kuleta matokea mazuri katika shule zao.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Profesa Eliamani Sedoyeka  amesema kuwa mafunzo hayo  ni moja kati ya mchango wa Chuo hicho kwa jamii kwa kuimarisha mifumo ya uongozi na usimamizi wa fedha katika shule za sekondari ili kuongeza ufanisi na kuchochea maendeleo ya elimu kwa ujumla.

Kwa upande wao Wakuu wa shule za sekondari Richard Mgabuso na Mary George Wamesema kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa walimu wakuu ambao in viongozi na wasimamizi wa fedha zinazotolewa na serikali juu ya namna ya kupanga na kutumia vyema fedha hizo.

No comments:

Post a comment