Thursday, 10 October 2019

Zaidi ya vyama vya ushirika 2000 nchini huenda vikafutwa kwa kutofuata sheria.


Happy Lazaro Arusha.

Zaidi ya vyama  2000 Vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Tanzania  {SACCOS) nchini huenda vikafutwa baada ya vyama hivyo kushindwa kufuata sheria na kanuni za Ushirika.

 Hayo yamesemwa na Kaimu Mrajisi wa vyama vya Ushirika Tanzania ,Tito Haule katika Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mkopo Kitaifa iliyofanyika Jijini Arusha.

Haule alisema kuwa ,Saccos nyingi zilifunguliwa katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuzitaka bilioni moja zilikuwa zikitolewa kama msaada na Rais baada ya kuzipata fedha hizo Saccos hizo sasa hivi haziko na wala havifanyi kazi kama sheria na kanuni zinazoelekeza. 


Alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni kila mwaka lazima kuitishwe mkutano mkuu na kusomwe taarifa ya mapato na matumizi na Bodi ya Saccos inapaswa kukaa vikao visivyozidi vinne na taarifa ya vikao hivyo mrajisi msaidizi wilaya na Mkoa anapaswa kuwa na nakala za vikao hivyo .

Kaimu Mrajisi alisema kuwa, katika kumbukumbu zake kuna Saccos zaidi ya 2000 hazifanyi vizuri kwa kukiuka taratibu hizo hivyo hawezi kuziacha lazima atazifuta kwa mujibu wa sheria ya nchi.


Akizungumzia ubadhilifu,Haule alisema kuna baadhi ya Saccos zinafanya vizuri na zingine zinavuja pesa za wanachama kwa makusudi ikiwa ni pamoja na Bodi kufanya vikao zaidi ya 25 kwa mwaka na kila mjumbe hulipwa shilingi 300,000 katika kila kikao kitu ambacho ni kinyume na sheria na kanuni za ushirika.


Haule alisema {bila ya kuitaja Saccos} kuwa alipohitaji muhutasari wa vikao hivyo 25 hakuweza kupata na mwisho wake alipata muhutasari wa vikao vinne tu na kusema kuwa viongozi wanapaswa kujitambua kuwa dhamana waliyoipta kuongoza wasiitumia kufuja pesa na kwa hilo hata mwacha mtu salama.


Alisema ofisi yake haita mwacha salama kiongozi wa Saccos atakayefuja pesa za wanachama kwani rungu la sheria litachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashitaka ya ubadhilifu.

 Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania{SKAUTI} ,Somoe Nguhwe alisema jukumu la kuongoza kwa kufuata sheria na kanuni ni la kila kiongozi hivyo kila mmoja anapaswa kuwajibika katika hilo.

 Nguhwe alisema ifike wakati iwe mwisho kwa viongozi kufuja fedha za wanachama ili kuleta sifa katika uongozi na wanaokula pesa hawataachwa kwani vyombo vya dola vinapaswa kuwachukulia hatua.

 Mwanachama kutoka Mkoani Ruvuma,Willbard Ngambeki yeye aliunga mkono kauli ya Mrajisi ya kuzifuta vyama vya Saccos vya mfukoni vilivyoanzishwa kwa malengo fulani kwani hivyo ndio vinaleta sifa mbaya kwa sasa kwani serikali ya awamu ya tano inaongozwa na Rais Dkt John Magufuli haina mzaha kwa hilo.

 Alisema kuwa,mbali ya changamoto zilizopo lakini zile Saccos za mfukoni ndio tatizo hivyo ni lazima serikali ifuate sheria na kanuni bila ya kuonea mtu ili vyama hivyo viweze kukubalika serikali.


No comments:

Post a Comment