Friday, 25 October 2019

WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII WAPEWA STADI ZA KUAMSHA ARI YA JAMII KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEONa Mwandishi Wetu Dodoma

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini wameaswa kutumia mbinu walizonazo kuleta ushawishi kwa wnanchi na kuwahamasiha katika kujitolea kushiriki katika shughuli za kimaendeleo katika maeneo yao.

Hayo yamebainika jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii uliwakutanusha Wataalam hao utoka Sekta za umma, Binafsi na Mashieika Yasiyo ya Kiserikali nchini.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii CODEPATA Bw. Sunday Wambura amesema kuwa Maendeleo ya Jamii ni mchakato unaowezesha watu kubadili fikra hasi kuwa chanya kuhusiana na maendeleo yao katika nyanja zote.

Bw. Wambura aliongeza kuwa Maendeleo ya Jamii ni mchakato kwa sababu huu unawezesha watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na kutumia fursa na rasilimali zilizopo kuboresha maisha kukuza kipato na uchumi wao kwa ujumla.

Aidha Bw. Wambura alieleza kuwa maendeleo endelevu na jumuishi yanasisitiza ushiriki wa jamii katika kuamua, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini na ili jamii iweze iwe na mtizamo chanya, kushiriki na kupokea mabadiliko anwai inahitaji ulaghabishi.

“Wataalam wa maendeleo ya jamii wanazo stadi za kutumia mbinu shirikishi zinazowezesha kuamsha ari ya jamii kushiriki katika maendeleo yao ikihusisha watu wote na makundi mbalimbali yaliyosahaulika katika jamii” aliisitiza Bw. Wambura.

Bw. Wambura amewakumbusha wanachama wa COPEDATA kuwa wataalum wa taaluma mbalimbali duniani hujipambanua  kupitia vyama vya kitaaluma na kuongeza kuwa uwepo wa vyama hivi umekuwa na tija kwa uimara na ubora wa taaluma husika pamoja na maendeleo ya Taifa kutokana na mchango wa vyama hivyo.

Bw. Wambura alisema kuwa ni jambo la tija kwa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuwa na chama cha kitaaluma kinachowaunganisha na kuwaongoza akiongeza kuwa chama chake bado ni kichanga kwahiyo kinahitaji hivyo kila mwanachama anaowajibu wa kukijenga.

“Mwelekeo wa Chama kuwa ni kuwa chama imara na chenye nguvu si kwa ajili ya kukinzana au kupambana na mamlaka au taasisi yoyote  bali kwa ajili ya kulinda , kutetea na kuweka viwango bora vya utendaji kazi  vya Wataalam wa Maendeleo ya Jamii’’. Aliongeza Bw. Wambura.Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wamemaliza Mkutano Mkuu wao wa mwaka Jijini Dodoma uliolenga kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.

MWISHO

No comments:

Post a comment