Wachezaji wa timu ya Kikapu ya Deepsea ya Jijini Tanga wakiwa mazoezini wakijiandaa na michuano ya Kikapu U -16  itakayoanza kesho kwenye uwanja wa JMK
 Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole kushoto akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari 

 Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole katikati akisisitiza jambo  kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari 
Kocha Mkuu wa timu ya Deepsea ya Jijini Tanga Ali Hassani Senkole akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wake mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Bandari 
NA MWANDISHI WETU, TANGA.

MABINGWA watetezi wa Mashindano ya Kikapu nchini U-16 timu ya Deepsea leo wamefanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea Jijini Dar es Salaam kesho kwenda kushiriki michuano hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Kidonge chekundu JMK.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo Kocha Mkuu wa timu hiyo Ali Hassani Seknole alisema kwamba maandalizi kwa upande wake yamekamilika kwa asilimia kubwa na wachezaji wapo tayari kuweza kupambana na kutetea ubingwa wao ambao waliuchukua mwaka jana.

Alisema kwamba anashukuru kutokana na matayarisho ambayo wameyafanya kwa kipindi cha muda mrefu wanaimani kwamba watafanikisha ndoto zao za kuweza kurudi na Ubingwa wa Michuano hiyo ambayo imekuwa na upinzani mkubwa kila mwaka.

“Kwa kweli tunashukuru maandalizi yamekwenda vizuri na hatuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi lakini kubwa tunawashukuru wafadhili mbalimbali ambao wametusawaidia kwa ajili ya timu yao kwenda kushiriki mashindano hayo kutoka Mwanza, Kigoma, Mtwara na Dar na Tanga”Alisema Kocha huyo

Hata hivyo alisema kwamba timu hiyo itaondoka na wachezaji 10, viongozi wawili huku akieleza kwamba wataanza mechi yao ya kwanza kesho jioni huku wakihaidi kuweza kupata matokeo mazuri.

Naye kwa upande wake Nahodha wa kikosi hicho Alex Clemence alisema wamejiandaa vizuri kwenda kupambana na adui wa aina yoyote ile ili kuweza kupata matokeo mazuri na kurudi na ubingwa
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: