Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewaondoa wasiwasi wakazi wa jiji la Arusha na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuijiandikisha katika daftari la wapigara kura la uchaguzi mdogo wa serikali za mtaa katika siku tatu ambazo serikali imeongeza hadi kufikia tarehe 17 octoba mwaka huu kwani jeshi hilo limeimarisha ulinzi na usalama wa kutosha kwa wananchi wote.

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan  Shana amesema kuwa kufutia serikali kuongeza siku za kujiandikisha jukumu lao ni kuhakikisha usalama kwa wananchi wote kwani jeshi litafanya kazi bila kupendelea chama chochote cha siasa.

Shana amesema kuwa serikali inawajali wananchi wake na kuamua kuwaongezea siku za kujiandikisha ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Kamanda huyo amesema kuwa jeshi hilo linafanya kazi kwa kuzingatia kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali katika kutekeleza wajibu wake wa msingi.

“Tunawaomba wakazi wa Arusha wajitokeze kwa wingi katika siku hizi zilizoongewa wajiandikishe kwa wingi na pia wajitokeze kupiga kura” Alisema Kamanda
Share To:

msumbanews

Post A Comment: