Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri mkuu mstaafu Mizengo Peter Pinda ameitaka Taasisi ya utafiti Wa kilimo Tanzania (TARI) katika kituo cha Makutupora mkoani Dodoma kuandaa kijitabu cha mwongozo Wa zao la zabibu.

Mhe. Pinda amesema hayo Leo Okt.27.2019 jijini Dodoma wakati akifunga hitimisho la tamasha la Urithi wetu Festival lililofanyika viwanja vya mashujaa jijini hapa.

Waziri mkuu mstaafu huyo amesema endapo kituo cha utafiti Wa kilimo Makutupora kitaanzisha kijitabu cha mwongozo Wa zao la zabibu itakuwa rahisi kwa wakulima Wa zao hilo kupata ujuzi zaidi Wa zao la zabibu na kuongeza mnyororo Wa thamani katika uzalishaji wake.

"Ili zao hili lilete tija Zaidi kwa wakulima niwatake kituo cha utafiti Wa kilimo cha hapa Makutupora kuandaa kijitabu cha mwongozo Wa zao la zabibu maana wakulima walio wengi hawana ujuzi Wa kilimo cha zao hili hivyo zao hili litaleta tija kubwa kwa wakulima" amesema.

Aidha Mhe. Pinda amesema kuhusu sifa ya Mkoa Wa Dodoma katika uzalishaji Wa zao la zabibu ,kutokana na yeye mwenyewe kuwa mkulima mkubwa Wa zao hilo amefuatwa na watu kutoka nchi za Ufaransa na Italy wakimwuliza siri ya zao hilo kustawi zaidi katika mkoa Wa Dodoma.

"Nimefuatwa na watu kutoka Ufaransa na Italy nini siri ya zao hili,nikawaambia Mimi sio mtaalam Wa kilimo wakafanya utafiti zaidi wakaja na majibu matatu ,kwanza udongo Wa Dodoma ni Wa aina yake na unahimili ukame,pili hali ya Joto la Dodoma halifanani na la jangwani ,na tatu mvua za Dodoma hazifanani na za Mkoa mwingine  Tanzania na Duniani kwa ujumla,ikimaanisha kuwa Dodoma ina kiwango kidogo cha mvua"
Pia Mhe. Pinda amewasihi wakulima kutoka tamaa kutokana na changamoto.

Hata hivyo,ametumia fursa hiyo kuzitaka taasisi za kifedha zikiwemo benki kupunguza masharti ya mikopo kwa wakulima na kuwataka wakulima kupata ushauri Wa usindikaji kutoka shirika la viwanda vidogovidogo    (SIDO)na kuwasihi kupata ushauri kutoka shirika la viwango Tanzania(TBS) pindi wanaposindika mazao yao.

Waziri mkuu mstaafu Mhe. Pinda ametaja miongoni mwa faida ya zao la zabibu kuwa ni pamoja na virutubisho muhimu kwa mwili Wa binadamu ikiwa ni pamoja na vitamin C na K
Kuhusu viwanda mkoani Dodoma,   amesema mkoa Wa Dodoma una viwanda 2341 na umetoa ajira za kudumu 23,470 na viwanda vinavyosindika zao la zabibu ni 12 tu kati ya hivyo vikubwa ni 2 na vidogo ni 10 na vina uwezo Wa kununua zao la zabibu kwa wasilimia 65% tu na asilimia 35% inategemea soko kutoka nje ya nchi hivyo bado kuna fursa kubwa ya zao la zabibu.


Kwa bei zabibu inauzwa kuanzia 1200 hadi 6000 kwa kilo kutokana na ubora wake.

Mwenyekiti Wa tamasha la Urithi Festival Prof.Martin Martin amesema lengo la tamasha hilo ni kukuza sekta ya utalii,huku Naibu Katibu mkuu Wizara ya maliasili na utalii Dokta Aloyce Nzuki akisema Urithi Festival ni kuhakikisha utamaduni haupotei na watanzania hasa wanadodoma  wanapata kipato na kuhakikisha pia zao la zabibu sio kwa biashara pekee bali hata kiutalii.

Naye mkuu Wa mkoa Wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amesema ardhi ya Dodoma ni dhahabu na ni ghala la chakula endapo yatatumiwa vizuri mazao yanayostawi katika mkoa huo.

Aidha,Dokta Mahenge amesema ukipanda zabibu zaidi ya mita moja kwenda chini unanufaika kuvuna kwa muda Wa miaka 60 hadi 70.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wote Wa wilaya mkoani Dodoma,mkuu Wa wilaya ya Chemba Simon Odunga amesema wilaya za mkoa Wa Dodoma zimejipanga kuhakikisha zinafikia mnyororo Wa thamani katika kukuza kilimo cha zao la korosho.

Katika tamasha hilo,wakulima bora Wa zao la zabibu wametunukiwa vyeti ambao Wa kwanza ni Ngwabi Investment, Wa pili ni Mama Majebele kutoka Hombolo.
Aidha,Vikundi bora vitatu vya ngoma vilijishindia zawadi ambapo mshindi Wa kwanza Tsh.laki 2,mshindi Wa pili Tsh.laki 1 na elfu 50 na mshindi Wa tatu Tsh.laki 1.

Marimbwende Wa Zabibu nao hawakuachwa nyuma ambapo miss zabibu Wa kwanza ni Paulin Willson amejishindia million 1,Wa pili ni Jesca Meshack amejishindia laki 4,na Wa tatu ni Winfrida Mondo amejishindia laki 3.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: