Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro ametoa tuzo kwa walimu bora wa shule za msingi na sekondari wa Wilaya ya Arusha mjini kwa kuweza kufaulisha wanafunzi katika alama za juu za ufaulu wa masomo mbalimbali hivyo kulifanya jiji hilo kufanya vyema katika matokeo ya kimkoa na taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Walimu  iliyofanyika katika viwanja vya Nane nane jijini Arusha na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Jiji la Arusha,shirika la The Foundation For Tomorrow ,Shule ya Lucy Vicent .ambapo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka walimu kuboresha mbinu za ufundishaji na kuwa wabunifu badala ya kufundisha kimazoea.

Gabriel amewataka walimu kujivunia kufaulisha wanafunzi katika alama za juu ikiwa ni pamoja na kujenga nidhamu miongoni mwa wanafunzi na walimu ambao ni walezi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr.Maulid Madeni amesema kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa walimu katika ujenzi wa taifa kwani walimu ni kada muhimu ambayo inashiriki katika kujenga taifa kwa kuzalisha wataalamu katika sekta mbalimbali.

Dokta Madeni ameeleza kushangazwa na risala ya walimu ambayo haikugusia mchango wa Mwalimu Nyerere katika kada ya Ualimu kwani alikua mwalimu na alifanya kada hiyo kuheshimika katika jamii ya Watanzania na ulimwenguni.

“Ndugu zangu Walimu katika awamu ya Tano Raisi John Pombe Magufuli amefanya mambo makubwa katika elimu ikiwemo kutoa elimu bure kwa watoto wa wa Tanzania na kuboresha miundombinu na mazingira bora ya kutoa elimu lakini hotuba ya walimu haijagusia hilo ni vyema kutambua mchango wa Raisi katika elimu” Alisema madeni

Katibu wa Chama cha Walimu jiji la Arusha (CWT) Abraham Kamwela akisoma risala ya Walimu amesema kuwa licha ya mafanikio waliyonayo bado wana changamoto mbalimbali ikiwemo madeni  ya mishahara,fedha za likizo pamoja na changamoto ya kukosa makazi ambapo wameliomba jiji la Arusha kuwapatia walimu viwanja kwa bei nafuu ili kuwawezesha walimu kujenga makazi yao na kujimudu kimaisha.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: