Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi aonya baadhi ya Watumishi wanaowanyanyasa wazee hususan watumishi wa afya wanaowalizimisha wazee kuchangia huduma za afya licha ya serikali kuelekeza wazee watibiwe bure.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya wazee katika shule ya parent Afisa tarafa huyo amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua watumishi wanaokiuka maelekezo ya serikali kwani serikali inathamini mchango wa wazee katika ujenzi wa taifa la Tanzania.

Titho ameahidi kuzishughulikia changamoto zinazowakumba wazee ili kuhakikisha wazee wote wanapata haki sawa


Wazee wa kata ya sokoni one jijini arusha wameiomba serikali kuwachukulia hatua watumishi wa vituo vya afya ambao wamekuwa wakiwataka wachangie fedha za matibabu licha ya serikali kutaka huduma hizo zitolewe bure kwa wazee. 

Gerald Machafuko na Tabu said ni miongoni mwa wazee walioshiriki katika hafla hiyo wao wamesema swala la kupatiwa matibabu limekuwa changamoto inayowasumbua wazee wengi jambo ambalo linawapelekea kushindwa kwenda katika vituo vya Afya kupatiwa matibabu kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

“Jicho langu lina matatizo mikono yangu ilikufa gansi yote miwili nilipoenda hospitali dirishani niliambiwa nilipe shilingi elfu thelasini mimi hiyo hela naitoa wapi na mmenipiga picha na kitambulisho mkanipa”Alisema mzee Tabu said kwa machungu.

Paul Moshi Ni mwenyekiti wa baraza la wazee katika kata ya Sokoni One yeye anaiomba serikali kuwajengea zahanati katika kata hiyo ili waweze kupata huduma za Afya kwa urahisi.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata hiyo amesema kwa sasa wameanza utaratibu wa kuwapatia wazee vitambulisho na hawajawahi kupata malalamiko ya wazee ambao wametozwa fedha pindi wanapoenda hospitali kupatiwa matibabu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: