Friday, 13 September 2019

Waziri Shonza apangua hoja ya TBC kubagua Vyama vya UpinzaniNaibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kwa TBC kubagua baadhi ya vyama vya upinzani jambo ambalo limepingwa vikali.

Shonza amesema kuwa yeye kama Naibu Waziri ameuhakikishia umma kuwa TBC ni chombo cha kila mtu kwasababu kinaendeshwa kwa kodi za Watanzania.

"Kuna malalamiko kwamba TBC inachagua baadhi ya Vyama katika Uendaji kazi wake,  mimi Naibu Waziri ninatumia kuwahakikishia kuwa TBC ni chombo cha umma nikisema chombo cha umma ni chombo ambacho hakina itikadi ya vyama," amesema Shonza.

"Kwahiyo upinzani wasisite kuleta habari zao katika chombo hiki cha umma na kinaendeshwa kwasababu ya kodi za Watanzania."

No comments:

Post a Comment