Tuesday, 17 September 2019

Waziri Angellah Kairuki atoa msaada wa Vyerehani 45



Na Ferdinand Shayo,Killimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji  Angellah Kairuki  amekabidhi msaada wa  jumla ya vyerehani 54 kwa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Same pamoja na jumuiya zake ikiwemo Umoja wa Wanawake (UWT),Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) pamoja na Jumuiya ya Wazazi.

Akizungumza wakati akikabidhi vyerehani hivyo ambavyo vitatumika kama mradi wa kuongeza kipato cha Chama cha Mapinduzi wilayani hapo pamoja na kupunguza utegemezi,Kairuki amewataka kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kufungua biashara ya ushonaji wa nguo .

Kairuki amekitaka Chama hicho kutumia vyerehani hivyo kama sehemu ya kutoa mafunzo ya ushonaji pamoja na kuvilinda ili viwasaidie .

Akipokea vyerehani hivyo vilivyotolewa na Waziri Kairuki Mwenyekiti wa CCM  wa Wilaya hiyo Bw .Isaya Mngulu amewataka viongozi wa ccm na jumuia hiyo kupanga matumizi sahihi ya msaada huo vizuri ili chama hicho kiweze kukua kiuchumi.

Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Senyamule amempongeza Waziri Kairuki kwa kujitoa kusaidia Wilaya ya Same katika masuala ya Afya,Vikundi vya Wajasiriamali pamoja uwezeshaji wa kiuchumi.

No comments:

Post a Comment