Sunday, 8 September 2019

Wananchi wametakiwa kuchangamkia fursa ya Ujenzi wa Stendi kubwa ya Mabasi ya Mkoa wa ArushaNa Ferdinand Shayo,Arusha.

Wananchi wa wanaoishi katika kata ya Olasiti wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotokana na ujenzi wa stendi kubwa ya mabasi ya mkoani katika kata hiyo itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 10 zilizotengwa na serikali.

Akizungumza katika mkutano na wananchi wa kata hiyo  Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi amesema kuwa wananchi hao hawapaswi kuwa nyuma katika kuchangamkia fursa za ujenzi wa kituo hicho kikubwa cha mabasi na badala yake watumie fursa hizo ambazo zinaketwa na serikali kwa lengo la kuwakomboa wananchi wake.

Cholobi amesema kuwa serikali imeleta fedha nyongi katika kata hiyo kwa ajili ya kutekekeza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara,nyumba za walimu ,madarasa  pamoja na maabara.

Diwani wa kata hiyo ameishukuru serikali kwa kuwaletea miradi ya maendeleo katika kata hiyo ambayo inalenga kutatua changamoto za wananchi ikiwemo miundombinu ya barabara pamoja na kutatua changamoto za elimu.

No comments:

Post a comment