Nchi yetu imepata heshima ya kupokea ugeni wa Mhe. Yoel Kaguta Museven Rais wa Uganda ambaye anatarajiwa kufika hapa nchini siku ya Alhamisi ya tarehe 05/09/2019 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 05/09/2019 hadi 07/09/2019.
Mhe. Yoel Kaguta Mseven atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport Terminal I na mwenyeji wake hapa nchini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli muda wa saa 12.00 jioni.
Mhe. Rais Museveni anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda. Aidha, Mhe. Rais Museveni anatarajia kuzindua rasmi jengo jipya la Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere lililopo katika Barabara ya Sokoine/Morogoro Dar es Salaam tarehe 6 Septemba, 2019.

Mgeni wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini tarehe 07/09/2019 na atasindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Tunaomba radhi kwamba njia atakazopitia mgeni wetu zitakuwa zinafungwa kwa muda ili kupitisha misafara ya viongozi wetu wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Mwl. J. K. Nyerere kumpokea Mgeni wetu hususani barabara ya Nyerere mpaka Mgeni wetu atakapokuwa amewasili na siku ya kuondoka.

Kwa kutambua ugeni huu sisi kama wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania tunamkaribisha mgeni wetu na ajisikie kuwa yuko nyumbani muda wote atakapokuwa hapa jijini.
Asanteni sana.
IMEANDALIWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
Share To:

msumbanews

Post A Comment: