Na. James Timber, Mwanza

Aliyekuwa mgombea Udiwani kupitia Chama Cha Chadema  Kata ya Chifunfu mwaka 2015  Malebo Ntalano pamoja na Mwenyekiti wa Bawacha, Riziki Juma amekihama chama hicho na kujiunga na CCM na kuisambalatisha ngome hiyo ambayo ilikuwa mwiba kwa CCM.

Amesema kuhama kwake Chadema kumetokana Rais kutimiza waliyokuwa wakiyatafuta wakati wakiwa chadema hivyo hakuna haja yakuwa Chadema tena.

''Nimeondoka Chadema na siludi tena sasa CCM ndiyo sehemu sahihi miradi inatekelezeka alisema  Ntalano.

Ntalano alisema.baada ya kuhama yeye amehama na zaidi ya wanachama 30 wa chadema ambao nao wamehamia chamacha mapinduzi.

Kwa upande wake Aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha kata ya Chifunfu Riziki Juma alisema kuwa kuhamia kwake CCM alichagua mahali.salama na penye heshima hivyo atafanya kazi kwa Uhuru na amani.

Katibu wa CCM tawi la Chifunfu Julias Mngele amekili kuwapokea wanachama hao na kukili wazi kuwa kuhama kwao CCM kumewapunguzia kazi kwenye uchaguzi bwa serikali za mitaa kwa kuwa wao walikuwa ni kikwazo Cha ushindi wa CCM.

Viongozi mbalimbali na wanachama wa Chadema wamekuwa. wakikihama chama hicho na kujiunga na CCM akiwemo diwani wa Kata ya Nyampulukano Emmanuel Munwazi na chama hicho kuwa kimekosa nguvu wilayani.sengerema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: