Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya

Sakata la upotevu wa kiasi cha Shilingi Milioni 76 za ada ya wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Moshi, lililopelekea wanafunzi hao kuandamana, limeleta sura mpya baada ya Bodi ya Shule, Benki ya CRDB na Mawakala wa benki hiyo kukaa na kuweka makubaliano ya kwamba kila mmoja awajibike.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Septemba 13, Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, ametoa siku 7 kwa Wahasibu waliohusika kwa kiasi kikubwa kufanya ubadhilifu wa fedha hizo kulipa Milioni 40, huku zingine Milioni 36 zikitakiwa kulipwa na taasisi zao ikiwemo  Benki, Chuo pamoja na mawakala wa ELCT -SACCOS.
''Mgogoro umeisha na tumekubaliana kwamba, wahusika wawili wanalipa Shilingi Milioni 40, taasisi zao wanalipa milioni 36 na nimewaambia wazilipe ndani ya siku 7'' amesema DC Sabaya.
Wanafunzi wa Chuo hicho waliandamana siku ya Jumatatu ya Septemba 9 na kushinikiza Serikali kuingilia kati sakata la utapeli wa zaidi ya Sh.milioni 75 za malipo ya ada ambazo hazionekani kwenye akaunti ya Chuo.
 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: