Mbunge wa Singida Magharibi, Mhe Elibariki Kingu ameupokea msafara wa kundi la wandishi wa habari wanaoenda nchini Burundi kuiunga mkono Timu ya Taifa 'Taifa Stars' katika mchezo wake wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Mhe Kingu pamoja na kuupokea msafara huo wenye watu 35 pia ameuandaliwa kifungua kinywa pamoja na kuchangia kiasi cha Shilingi Laki Mbili kama sehemu ya kuunga mkono kampeni hiyo ya kuhamasisha Timu ya Taifa.

" Niwashukuru Sana ndugu zangu wanahabari kwa kuamua kujitolea kuunga mkono Timu yetu ya Taifa. Historia lazima iwakumbuke mmefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa hapo awali. Nyinyi ni mashujaaa wa Taifa hili.

" Niwahikikishie Mimi ni sehemu ya kampeni yenu, nitashirikiana nanyi kwa kila Jambo, lengo likiwa kumuunga mkono Rais wetu Dk John Magufuli kupitia Michezo na haswa Timu yetu ya Taifa. Twendeni pamoja.," Amesema Mhe Kingu.

Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na wandishi wa habari za michezo na ilianza katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, dhidi ya Kenya ambapo Taifa Stars ilifuzu kwenda hatua inayofuata.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: