Timu ya madaktari kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha wamezindua huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito katika  kituo cha afya Daraja Mbili kilichopo Jiji la Arusha.
Akiongoza zoezi hilo Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha amesema kuwa kuzinduliwa kwa huduma hiyo kutawapunguzia wananchi gharama kwa kuwa huduma hiyo ni bure katika vituo vya  afya vya  serikali ukilingalinganisha na vituo vingine.
Dkt. Chacha ameongeza kuwa licha ya kupunguza gharama  kwa wananchi lakini pia kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kupunguza msongamano kwa mama wajawazito kujifungulia katika hospitali za mjini kama vile hospitali ya rufaa ya Mount Meru.
“Kwa sasa hivi huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito inapatikana katika vituo vya afya vitatu vya Jiji la Arusha ambavyo ni Kaloleni, Levolosi na Daraja Mbili na kituo kinachofuata kuzinduliwa huduma hii ni Murriet” alisema Dkt. Chacha


Timu ya madaktari wa kituo cha afya Daraja mbili  katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha (wa tatu kutoka kulia) baada ya kukamilisha upasuaji wa kwanza
Share To:

msumbanews

Post A Comment: