Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro ameabidhi msaada wa magodoro,vyandarua,chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu kwa kaya 13 ambazo hazina makazi baada ya nyumba waliyokua wakiishi kuteketea kwa moto katika Mtaa wa Migungani ,kata ya sinoni  jijini Arusha .

Akizungumza na wahanga hao wa janga LA moto ,Gabriel amesema kuwa serikali imesikia kilio chao na kuwasilisha mahitaji ya haraka yaliyotolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao katika kipindi hiki kigumu walichopo kwani wanahitaji msaada wa haraka ili waweze kurejea katika majukumu yao ya kila siku.

Afisa Tarafa ya Elerai Titho Cholobi amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya nyumba hiyo kuungua moto walifika na kufanya tathmini ya mahitaji ya haraka na walipofikisha tathmini hiyo kwa Mkuu wa Wilaya walipata mahitaji hayo ambayo yatawasaidia wananchi.


Cholobi amesema kuwa serikali ya Dokta John Pombe Magufuli itaendelea kuwasaidia wananchi hao na kuwaomba wadau wengine wakitokeze ili kusaidiana na serikali.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wahanga  hao Aurelia Matson ameishukuru serikali kwa msaada huo kwani kabla ya msaada huo hali ilikua ni ngumu kutokana na vitu vyao kuteketea kwa moto.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: