Florah Mgonja Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akiwa katika ofisi za Utamaduni Jijini Arusha

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Baraza la sanaa nchini lipo mkoani Arusha kwaajili ya kuratibu shughuli zote za sanaa ,kwa maana ya usajili na uratibu wa wadau kwa ujumla wakiwemo wamiliki wa kumbi,bendi ,studio ,washehereshaji,DJ,waandaaji wa matamasha pamoja na matukio mbalimbali ya sanaa kanda ya kaskazini.

Florah Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini amesema   baraza hilo limeanzishwa kwa mujibu wa sheria no 23 ya mwaka 1984 ,na kanuni zake za mwezi February 2018, zinawatambua wasanii pamoja na kazi zao ,pia zinamtambua Afisa utamaduni kanuni ya mwaka 2018 kipengele cha 22,kinamtanbua Afisa huyo kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa.

Amewataka wasanii kwenda kujisajili ili waweze kuhudumiwa sambamba na kauli mbiu ya Basata inavyosema kuwa sanaa ni kazi na  kama zilivyo kazi nyingine hivyo ni vyema wakajisajili ili watambulike .

Mgonja amesema wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanasajiliwa na hawaoni faida,watambue kuwa faida zipo nyingi kwani Basata lipo dawati ambalo msanii hupewa fursa mbalimbali, na kazi zao namna zinaweza kulindwa kisheria.

“Vipo vinandaumiza vingi ambavyo vinachukua kazi nyingi za wasanii,kama umesajiliwa serikali ipo kwaajili ya kuangalia haki ya msingi ya msanii na tunaishughulikia kwa namna gani ili msanii aweze kusonga mbele”alisema Flora.

Mratibu huyo wa kazi za sanaa kanda ya kaskazini, amesema kuwa kwa sasa wapo wanatoa elimu kwa wasanii na vikundi mbalimbali,ila wakati unakuja kwa wasanii ambao hawatajisajili sheria itachukua mkondo wake .

Aidha amesema Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia  kupitisha Sheria amabayo itawabana wasanii ili kuwasaidia kiuchumi badala ile ya Mwanzo ya mwaka 1984 sheria No 23 kuwa na mapungufu.

Florah Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akisisitiza jambo kwa waandishi wanhabari (hawapo pichani)katika ofisi Utamaduni Jijini Arusha.
Aidha amesema kulikuwa na malalamiko juu ya COSOTA,BODI YA FILAMU,BASATA kutokana na utendaji kazi wake kwani msanii alikuwa kote anatozwa kwa sasa serikali imaangalia namna gani hizi Taasisi tatu zinakuwa mamlaka ya usimamizi wa kazi za sanaa ambapo michakato tayari imeshaanza na inaratibiwa na TCRA.

Amesema kwa wale wote a,mbao wanafanya kazi bila kusajiliwa sheria itafuata mkondo wake kwasababu kwa sasa Basata ipo katika kuelimisha ,itafika mahali tukishaeka mambo sawa ikiwemo sheria na hizi mamlaka kuwa pamoja ,tutahakikisha kuwa kila anayejihusisha na shughuli za sanaa anasajiliwa.

Amesema zipo faida nyingi za msanii kujisajili ikiwemo sheria,kazi zao kutunzwa kupata fursa mbalimbali huku akiwataka wale ambao wameshajisajili kuhuhisha vibali vyao ,kwa msanii binafsi ni shilingi 45,000 kwa vikundi 85,000 ikiwa imejumlishiwa na fomu.

Amebainisha kuwa kwa sasa msanii hawezi kwenda nje ya kwa kupitia viwanja vya ndege  nchi kama hajasajiliwa Basata,hivyo umuhimu wa kujisajili ni mkubwa, kwani hata msanii akipata shida akiwa nje ya nchi ni rahisi kusaidika kama amesajiliwa.

Amesema Basata ipo kwaajili ya kushughulikia usajili kwa wasanii sambamba na ushauri wa namna ambavyo wanavyoweza kuendesha shughuli zao za sanaa kwani fursa zipo nyingi sana.

Aidha Basata ilianza usajili kwa mwaka wa fedha 2018-2019 na usajili ulikuwa mzuri na wasanii waliitikia kwa wingi,hivyo kwa mwaka huu wengi wanahuisha vibalivyao kwa wale waliokwisha sajiliwa tayari ambapo wamekuwa mabalozi kwa wengine .

Ameeleza kuwa kwasasa Basata imewarahisishia kazi wasanii,badala ya kwenda Jijini Dar es salaam imewafuata hadi mkoa husika kwaajili ya kuwafanyia kushughulikia usajili wao .

Hata hivyo ameeleza kuwa msanii anapojisajili 25% ya makusanyo katika usajili huu unarudi halmashauri kama sehemu ya uendelezaji wa shughuli za sanaa.

Mwisho
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: