Na Issa Mtuwa “WM” Nanyumbu Mtwara
Sikuzote katika sehemu ya maisha yangu nikiwa kama Waziri wa Madini, hakuna kitu kinachonisononesha na kunikosesha amani moyoni kama ninapofika mahali au kuona kwenye vyombo vya habari wananchi tena wanyonge wanalia na kunyanyasika kisa wanakosa  maeneo ya kuchimba, wanalilia leseni ama mwekezaji wana wanyanyasa wakati rasilimali hizo zinawazunguka kwenye maeneo yao. 



Haya yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko tarehe 12/08/2019 wakati akiongea na wananchi wa kata ya Michiga wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kufuatia ziara yake wilayani humo kukagua shuguli mbalimbali za sekta ya madini na kutatua wananchi wanamlilia na kumpigia magoti kuomba eneo baba chondechonde tunaomba tusaidie eneo lile tuchimbe. 


Katika ziara yake katika mikoa ya Lindi na Mtwara Biteko amekutana na kilio cha wananchi karibu kila mahali kukosa maeneo ya kuchimba madini huku raslimali hizo zikiwa zimewazunguka. 


“Mhe. Waziri kuja kwako leo tunakushukuru sana, Babaa kiliochetu sisi ni eneo la kuchimba baba tafadhali chondee tunaomba turuhusu tukachimbe, tupate riziki babaaaa, pale palipo fungiwa hata sisi tunaathirika kwa sababu palikuwa panatusaidia” alisema Mzee Faya Bozani Mussa  alipopata fursa ya kuongea mbele ya waziri Biteko. 


Kufuatia kilio hicho akiwaangalia kwa huruma na kwa kuonyesha kuguswa na wananchi hao waziri Biteko papo hapo hakutaka kuwa chukuwa muda kutatua kero hiyo alitoa kauli na iliyo geuza huzuni kuwa furaha ya wananchi walio kusanyika kwa wingi katani hapo. 


“Ndugu zangu, poleni sana, naumia sana moyoni kuwaona mnasononeka moyoni kwa ajili ya raslimali zinazo wazunguka. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anawapenda sana na mimi ameniteuwa kumsaidia lakini kazi yangu aliyo nituma ni kuja kutatua kero za wananchi katika sekta ya madini na ndio maana nipo hapa Michiga siku ya leo.”  


“Mimi ni mtumishi wenu, nipo hapa kuwatumikia sipo teyari kuondoka hapa huku bado machozi yakiwa yanaendelea kutiririka. Sasa nisikilizeni. Moja, naagiza Tume ya Madini ifikapo ijumaa ijayo tarehe 16/08/2019 leseni ya lile eneo iwe imeshafika kwa Mkuu wa Wilaya ili yeye na afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mtwara waje wakabidhi hiyo leseni. Pili, safari yangu nimeambatana na Mkurugenzi Ukaguzi Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga yule pale, yeye atabaki hapa hataondoka japo kesho ilibidi aondoke kwa ajili ya majukumu mengine lakini hataondoka ili yule mwekezaji wenu Arafati Mrope  amsaidie kuandaa mpango kazi wa lile eneo ili ikifika leseni kazi ianze. Dkt. Utabaki hapaa” alisema Biteko. 


Maelezo hayo yaliibua shangwe, vigelegele, nderemo na vifijo kwa Wanamichiga na kusahau kilio chao. 


Kufuatia kauli hiyoo Mwenye (Chief) Njawala alisimama na kuishukuru serikali na kuipongeza huku akisema kauli ya waziri imeondoa minong’ono iliyokuwa imetanda ikiwatuhumu viongozi wa ngazi mbalimbali kuwa ndio waliokuwa wanawazuia wasichimbe wakati taratibu za kuchimba zilikuwa hazijazingatiwa. 


“Mhe. Waziri Mimi ni Chief wa eneo hili, nakushukuru kwa kutatua tatizo hili na umeleta amani maana awali viongi mbalimbali ndio walio kuwa wanatuhumiwa kwamba ndio wanaozuia, binafsi nakushukuru sana” alisema Chief Njalawa. 


Eneo  Michiga limezungukwa na madini ya Chuma eneo ambalo lilikuwa limechukuliwa na mwekezaji Arafati Omari Mrope aliekuwa anachimba na kununua madini hayo kutoka kwa wananchi na baadae eneo hilo kuzuiwa na serikali kwa kuwa waliokuwa wanafanya shuguli hizo walikuwa wanafanya kinyume cha sheria. 


Kwa upande mwingine Waziri Biteko alimshukuru na kumpongeza mwekezaji Arafati kwa kwa utii kwa serikali kwani hata alipo simamishwa asiendelee na kazi ya uchimbaji wa madini hayo mpaka afuate utaratibu kwa maana apate leseni alikubali na hakuendelea huku akilipa madeni ya zaidi ya Tsh. 35,000,000/= kwa wananchi waliokuwa wanachimba mchanga wa madini ya Chuma na kumuuzia mwekezaji huyooo. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alimshukuru Waziri wa Madini Doto Biteko kwa kufanya ziara hiyo na kutatua kero hiyo papo hapo bila kusubiri. 

“Mhe. Waziri nakushukuru sana kwa ujio wako, na maamuzi ya papo kwa papo na hiyo ndio speed ya serikali ya awamu ya tano katika kutaatua kero za wananchi hasa katika kufanyaa maamuzi yanayogusa maisha ya wananchi  wetu moja kwa moja” alise Machali. 

Kabla ya mkutano huo Biteko alikutana na kufanya kikao cha ndani na viongozi wa Wilaya ya Nanyumbu wakiongozwa na mkuu wa wilaya Moses Machali ambapo alisomewa taarifa ya wilaya kuhusu hali ya sekta ya madini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: