Monday, 5 August 2019

Wakulima Wametakiwa Kuepuka Matumizi Mabaya ya Viuatilifu


Na Ferdinand Shayo,Arusha
Mkuu wa wilaya ya mbulu mkoani manyara,celestine mofuga,amewataka Wakulima nchini kuepuka matumizi  mabaya ya viuatilifu ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata walaji ikiwemo magonjwa ya saratani .
Akizungumza jijini arusha wakati wa maonesho ya wakulima nanenane kanda ya kaskazini ambayo yamejumuisha mikoa mitatu,mofuga ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa manyara alipotembelea banda la taasisi ya udhibiti na usimamizi wa viuatilifu nchni (TPRI ),amesema ni vema wakulima kabla hawajanunua viuatili wakapata elimu namna yakutumia ili kujiepusha na madhara.
Maonesho ya wakulima nanenane jijini ausha ambayo yamejumuisha mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo i arusha,kilimanjaro na manyara ambapo mkuu wa wilaya ya mbulu,celestine mofuga ametembelea maonesho hayo.
mkuu wa wilaya ya mbulu,celestine mofuga ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa manyara,amewataka wataalamu taasisi ya udhibiti na usimamizi wa viuatilifu nchni-tpri-kutoa elimu kwa waulima ili waweze kuepuka matumizi mabaya ya viuatilifu ambayo yanaweza kuleta madhara .
kwa upandea wake mkuu wa wilaya ya simanjiro,zephania chaula, amewataka wataalamu kujenga mfumo wa kudhibiti magonjwa ya mimea kabla hayajawaathiri wakulima na kuwasababishia hasara kubwa ili wakulima waweze kulima bila kupata usumbufu wa wadudu vamizi.
afisa mazao wilaya ya hai mkoani kilimanjaro,zephania gundah,amesema tayari wana kliniki ya kutoa elimu kwa wakulima kuhusu  matumizi ya sumu katika kilimo ili kuepuka madhara ya kiafya na kuepuka kutumia gharama kubwa kwenye kilimo.

No comments:

Post a Comment