Mhadhiri msaidizi wa Chuo cha ustawi wa Jamii Abigail Kiwelu kutoka idara ya taaluma ya ustawi wa jamii na Afisa ustawi wa Jamii Subisya Kabuje kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi (wenye makaratasi) wakizungumza na mama mzazi (wa kwanza kushoto) na dada (wa pili kushoto) wa mmoja wa wahanga aliyepoteza maisha kwenye ajali ya moto msamvu.
………………
Timu ya wahadhiri na wanafunzi wa Chuo cha ustawi wa Jamii ikiongozwa na Mkuu wa taasisi hiyo Dkt. Joyce Nyoni wapo mkoani Morogoro kuanzia leo tarehe 13/08/2019 kuungana na timu ya maafa ya Mkoa wa Morogoro kutoa huduma za unasihi na huduma nyingine za awali za kisaikolojia kwa kuanzia na utambuzi wa mahitaji ya kisaikolojia ya wanafamilia hao.
Kwa kushirikiana na wataalamu wengine waliopo katika timu hiyo, Chuo cha Ustawi wa Jamii kitashiriki katika kupanga huduma na utekelezaji wa mpango wa huduma kwa familia hizo.
Katika kufanikisha zoezi hili timu ya maafisa ustawi inafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu sana na serikali za mitaa kuhakikisha kila kaya iliyofikwa na msiba au kupata majeruhi ya ajali hii mbaya ya moto zinatambuliwa mahitaji yao ya kisaikolojia na kupata huduma stahiki.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: